Mhubiri: Mchungaji Kiongozi Mhini
Maandiko: Matendo 2:42-47
Moja ya maagizo ni Meza ya Bwana au Ushirika Mtakatifu. Tunapaswa kuangalia mwanzo wa kanisa na baada ya pentekoste walishiriki
vipi Meza ya Bwana. Awali ya yote ya maagizo ya kanisa
tuliyoagizwa na Yesu mwenyewe hayapaswi kusahauliwa, kwa mujibu wa Meza
ya Bwana soma mathayo 26:26-30, hapa tunaona Bwana alihuzunishwa
sana moyono mwake kwasababu alikuwa anajua kinachoenda kutokea kwahiyo
akawakusanya wanafunzi wake katika meza akashukuru akaugawa mkate kwa wanafuzi
wake akasema twaeni mle huu ndio mwili wangu kwahiyo mkate ni alama ya mwili
wa Yesu. Unapokula mkate tambua unakula mwili wa Yesu, Yesu
alijua mwili wake utaenda kutundikwa msalabani lakini aliona kabla ya muda
ule haujafika ngoja aache alama ya mwili wake na huo ndio mkate uliomegwa na divai ni alama ya damu yake aliyomwaga pale msalabani.
Ni muhimu kushiriki Meza ya Bwana kwasababu ni sadaka yake
kwa ajili ya ukombozi wa wanadamu. Kwahiyo unaposhiriki
Meza ya Bwana usichukulie kama ni kitu cha kawaida na kushiriki Meza ya Bwana ni
amri, kama wewe umeokolewa unapaswa
kushiriki Meza ya Bwana. Kuna wengine muda wa kushirikki wanatoka nje ya
kanisa sasa inashangaza ni kwanni unatoka nje na unaacha kushiriki Meza
ya Bwana. Leo nakukumbusha kwamba kushiriki Meza ya Bwana ni amri kutoka kwa Bwana.
No comments:
Post a Comment