''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, April 6, 2014

UJUMBE: KUMLILIA MUNGU KATIKA SIKU ZILIZOHARIBIKA. 
Mhubiri: Mchungaji Mhini
Maandiko: Nehemia 1:1-7

Nehemia allikuwa mtumishi wa Mungu aliposikia malango ya mji wake Yerusalemu aliumia sana na akaketi na akalia sana na kuomboleza kwa Mungu wa mbinguni akimsihi Mungu wa mbinguni wa kuogofya amsikie maombi yake, na kumbuka hapo alikuwa utumwani lakini alikuwa akikumbuka habari za nyumbani kwao na akaanza kuiombea Yerusalemu. Alikuwa akipiga picha kichwani mwake kwamba mageti ya Yerusalemu na kwamba yamechomwa na waliobaki walikuwa wanawake na watoto kwasababu wanaume walichukuliwa mateka kwenda utumwani, na hekalu lilikuwa limesha bomolewa, kwahiyo picha ya nyumbani ikaanza kumjia. 

Nehemia alivyoyaona hayo akaingia kwenye zamu yake yaani ya maombi, kwahiyo na sisi kama watu tunaomjua Mungu tunavyoliona hili taifa letu halipo kwenye hali nzuri, ili hata yale majaliano ya bungeni yawe kwa ajili ya kumnufaisha mwanachi na sio kwa wasilahi yao, mali zetu zimetaifishwa kwa njia zisizoeleweka, kwahiyo wewe kama mtu wa Mungu unapaswa kukaa katika zamu yako na kuamua kuingia katika maombi. Vijana wengi sasa hawana kazi. 

Huzuni za Nehemia zilimfanya aingie katika maombi ya kumaanisha ya kufunga, na wewe leo kutokana na mambo mabaya yanayoendelea nchini yakuume na uamue kuomba na kufunga kwa kumaansha kwa ajili ya inchi yetu. Hebu tuingie kwenye maombi na chukua mzigo huu wa kuomba kwa kumaanisha, 2wakoritho 7:14-15, Lazima uwe mnyenyekevu na  kusoma Neno la Mungu ili uweze kumualika Mungu. Ingia kwenye zamu yako ibee nchi yetu, kanisa letu, familia yako na wewe mwenyewe, na ninaamini kwamba kama utaamua kubeba mzigo huo Mungu ataonekana katika maisha yako. Misihi Bwana Yesu kwa habari yako mwenyewe, tubu kwa ajili ya kanisa, tubu kwa ajili ya taifa.

No comments:

Post a Comment