UJUMBE: MALENGO MATANO ALIYOKUSUDIA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO
MHUBIRI: Mr. Benard Okech
1. Ulikusudiwa kwa ajili ya Furaha ya Mungu (KUABUDU) Isaya 61:3-5, Ufunuo 4:11
Mungu aliumba viti vyote na kwa mapenzi
yake vilikuwako, Mungu alitaka uwe hai na kufika kwako duniani na kapata burudisho.
Mungu amekuumba ili ujaze jamii yake kwa
kuwa mwaminifu, mnyenyekevu, mwenye adabu na mtu asiye toa siri za wengine.
3. Uliumbwa ili ufanane na Kristo, Mwanzo
1:26-27, Warumi 8:29
Katika uumbaji woote wa Mungu ni binadamu
tu ndiye aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mungu alituumba na kutuwekea roho ndani
mwetu kama Yeye alivyokuwa Roho, pia
akatupa uwezo wa kufikiri na kutatua matatizo mbalimbali, ametupa busara, uwezo
wa kupenda na kupenda, na wenye busara na uwezo wa kujua mema na mabaya.
Kila uwezo ulionao unaweza kuutumia kwa
ajili ya Utukufu wa Mungu. Kila mtu amepewa uwezo flani na Mungu na pia una
uzoefu mbalimbali kutokana na maisha uliyopitia, inawezekana ni uzoefu uliopata
kutokana na jamii unayoishi nayo, au elmu uliyonayo, kazi uliyonayo au hata
kutokana na karama uliyonayo. Uwezo au uzoefu huo unaweza kuutumia kuwahubiri
watu waliopitia katika hali hizo.
5. Uliumbwa kwa ajili ya Utume
Utume wako ni muendelezo wa utume wa Yesu
hapa duniani. Unaweza kutumia shuhuda
zako mbalimbali kushuhudia watu wanaopita katika hali kama hizo, mfano unaweza
ukamuelezea mtu jinsi Yesu alivyokuokoa naye akashawishika kuokoka.
No comments:
Post a Comment