Mhubiri: OBADAH MSAKI
Maandiko: Wafilipi 3:13-14
Mungu ni Roho, kwahiyo tunatakiwa
kumuabudu Mungu katika roho na kweli, ulipokuwa mdogo unakumbuka wazazi
walikuwa wanakuita na ukaanza kugundua kuwa ni wewe ndo unaitwa na
ulivyoendelea kukuwa marafiki zako wakaanza kukuita na wanavyokuita walitegemea
uitike, na ukiitwa na baba labda unakimbia, lakini leo tunaongolea wito wa
kuitwa na Mungu. Wafilipi 3:13-14, Paul
alihakikisha siku ile atakuwepo pale, na hii ndio mwito wa Mungu Waebrania 3:1,
Paul anaongolea wito, sio wito kutoka hapa duniani, wala sio kutoka kwenye mwezi
bali ni kutoka kwa Mungu mwenyewe, kuna sehemu 365 zinazosema usiogope lakini
kwenye hii Ebrania 3 anasema uogope, uogope kwasababu ukikosa huu wito utakuwa
huna sehemu ya kwenda.
No comments:
Post a Comment