Mhubiri: Mr. Frank Mwalongo
Maandiko: Mathayo 19:21-30
Tumeokolewa ndio lakini dhamani ya wokovu wetu ni nini? Kwahiyo tukijua
dhamani ya wokovu wetu nini hiyo
itafanya tuulinde zaidi kama una dhamani ndogo tutakuwa hatuna haja ya kuulinda
lakini kama una dhamani kubwa lazima tuutunze kwa gharama yoyote.
Mathayo 19:21-30, wakati huu Yesu
alitaka wanafunzi wake wajue dhamani ya wokovu wao, kwahiyo akaanza kuongelea
maswala ya yule tajiri, Yule tajiri aliyekuwa ana kila kitu na aliyesema
amefanya kila kitu kwa ajili ya kuurithi ufalme wa Mungu, umefanya vitu vingi
ndio lakini nenda kauze mali zako zote halafu unifwate, kwasababu Yesu alijua
Yule tajiri alikuwa anategemea ule utajiri wake alikuwa anaabudu utajiri wake,
kwahiyo akawa ana mwambia umefanya kila kitu ndio na kwasababu wewe ni tajiri
ili unifwate kauze mali zako zote na ugawie masikini kisha badae unifuate.
Yesu alipokuwa anaongelea swala
hilo kwa wanafunzi wake wanafunzi walishangaa alipomaliza kuongea na yule
tajiri akaja kwa wanafunzi wake akawaambia wanafunzi wangu ni ngumu sana kwa
tajiri kuingia mbinguni na ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano
ukilinganisha na tajiri kwenda mbinguni, na Yesu alisema hivyo ni kwasababu ya matajiri
kuabudu utajiri wao, Yesu hasemi kuwa hatufai kuwa matajiri lakini ukiwa tajiri
na unaabudu utajiri wako nenda kauze mali zako ili uweze kumuabudu Yesu ndomana
Yesu alisema hivyo. Alitaka wanafunzi wake wajue dhamani ya wokovu, inafaa ujue
uwe tayari hata kuuza mali zako zote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Yesu aliwaambia hivyo wanafunzi
wake kama kuwapa changamoto na akawaangalia machoni kwasababu alijua hata
wanafunzi wake watakuwa na hiyo shida na wanafunzi wake wakashangazwa sana na
wamafunzi wake wakajibu kwendana na mtazamo ule kwamba wauze mali zao alafu wamfuate Yesu, sasa
wakamwambia Yesu tumeacha mali zetu kazi
zetu Je! Sisi tutapata nini? Sisi tutapata nini Yesu? Na Yesu alikuwa anataka
waulize hilo swali, na anahitaji wewe uulize hilo swali kwamba umeacha kila
kitu je utapata nini na jibu la hilo swali ni kuhusu udhamani wa wokovu wetu,
tumeokolewa ndio lakini tunapata nini, na Yesu akawaambia wanafunzi wangu
nawaambia ukweli nitakapoketi kule kwenye kiti cha Enzi kuhukumu makabila 12
nyie mtakaa nami, na hilo ndio lilikuwa jibu. Kama umeokolewa na unaishi maisha
ya utakatifu Yesu anakwambia atakapokaa katika kiti cha Enzi utakaa pamoja na
Yesu. Ukisoma kitabu cha Yohana 3:18, 5:24, Yesu hakuja kuhukumu ulimwengu bali
kuokoa na wale walio okolewa hawata hukumiwa kwasababu tayari wana uzima wa
milele lakini wale waliomkataa wamekwisha kuhukumiwa kwasababu wameukataa
wokovu. Pia akawaambia wanafunzi wake chochote walichokiacha na kumfuata Yesu
watazidishiwa mara 100. Kwahiyo chochote ulicho acha kwa ajili ya Yesu utapata mara
mia lakini si hicho tu bali na Uzima wa milele.
Mr. Frank Mwalongo akiwa anahubiri |
No comments:
Post a Comment