''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, September 28, 2014

UTAUWA PAMOJA NA KURIDHIKA NI FAIDA KUBWA

Mhubiri: Dr. Makenzi
Maandiko: 2Samweli 9:1-13

Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani?. Roho Mtakatifu anauliza je amesalia hata mtu mmoja nipate kumtendea mema wakati huu?, mimi ntamjibu nipo hapa Bwana, tamani kutendewa mema ya Mungu wakati huu. 

Ukiendelea mstari wa 2-3 " 2. Palikuwa na mtumishi mmoja wa nyumba ya Sauli, jina lake Siba, basi wakamwita aende kwa Daudi; na mfalme akamwuliza, Wewe ndiwe Siba? Naye akasema Mimi, mtumwa wako ndiye. 3. Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu. Siba ambaye ni mfanya kazi tu alimtambulisha mtoto wa Yonathani kwa udhahifu wake 'kilema cha mguu', Yawezekana watu wanakutambulisha kupitia udhahifu wako. 

Lakini ukiendelea "4 Mfalme akamwambia, Yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Tazama, yumo katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari." Japokuwa siba alimtambulisha vibaya mtoto wa Yonathani lakini akauliza yuko wapi?, hata kama wamekutambulisha kwa kutumia udhahifu wako lakini Mungu anauliza yuko wapi ili apate kukutendea mema ya Mungu.


No comments:

Post a Comment