Maandiko: Yohana 17:20-23, Zaburi 133:1-3
Mhubiri: Mzee kiongozi, Dr. Mumghamba
Umoja kati yetu, umoja
kati ya familia na umoja kati ya kanisa, huwezi kuwa na umoja na mwenzako kama
hujamsamehe au kama una kinyongo nae, na kama una kinyongo na mwenzako hutaweza
kumshirikisha jambo lako mwenzako. Yesu
aliongelea umoja kama kitu muhimu sana katika maisha yetu na zaidi sana kwa
sisi tunaomwamini. Yesu alituombea kwa Mungu tuwe na umoja ndani yake kama Yeye
na Baba yake walivyokuwa wamoja. Umoja katika Yesu na sio umoja pamoja na Yesu,
alitaka wewe uwe ndani Yake na Yeye ndani yako ili wote tuwe na umoja katika
Yeye (Yesu) na tukishakuwa wote wamoja katika Yesu ulimwengu utaona kazi kubwa
aliyokuja kuifanya na ya kwamba Mungu alitupenda sisi sana kama alivyompenda
Yesu mwanae.
Kanisani mnaonana na
kukaa wote pamoja lakini yawezekana hamna umoja kati yenu wote, mume na mke
wanaweza wakaishi pamoja lakini yawezekana hawana umoja kati yao, familia
yaweza kuishi pamoja lakini wasiwe na umoja kati yao. Kwahiyo kukaa pamoja au
kuishi pamoja sio mara zote ikamaanisha umoja kati yenu.
Yesu alivyoongelea
umoja hakumaanisha umoja huu wa kawaida lakini umoja wa kiroho ambao ndani ya
umoja huo tunapata kubarikiwa na pia kuwa na uzima tele (zaburi 133:3).
Ukimruhusu Yesu kukaa
ndani yako na wewe ukikaa ndani yake kisawasawa hutapata shida wala hutasukumwa
na mtu kumpenda mwenzako, kama kila mtu katika familia au kanisa akikaa ndani
ya Yesu na Yesu ndani yao moja kwa moja familia au kanisa litakuwa na umoja.
No comments:
Post a Comment