''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, June 28, 2015

KITU CHA AJABU KINATOKEA KATIKA MAISHA YAKO

Mhubiri: Dr. Elifuraha Mumghamba
Maandiko: Kutoka 3:1-24

Musa alishangaa kuona kijiti kinachoungua lakini hakiteketei. Mungu alitaka na anataka ujifunze kitu kutoka kwenye kitu kisicho cha kawaida lakini ni mpaka uwe kiroho vizuri ndio utaona na kuelewa kitu/jambo fulani kutoka kwenye kitu kisicho cha kawaida.
 
Siku hizi watu wamekuwa busy busy sana na ni kweli uko busy lakini hata kama ukichoka lazima ujitaidi ule chakula cha usiku huwezi acha lakini utaona hauna muda wa kusoma Neno la Mungu ambalo ndio chakula cha roho yako. Hebu jaribu kuhesabu mara ngapi unashindwa kula chakula cha usiku kwasababu umechoka? ni mara chache sana lakini Je ni mara ngapi umeacha kusoma biblia na kuomba kwasababu ya kuchoka? labda ni mara nyingi.
 
Ufunua 12:11-12 kutoka katika neno hili tunaona kitu cha ajabu inasema shetani anajua muda wake ni mchache lakini kanisa au wewe unaona kuwa bado kuna muda mwingi tu hapa duniani kabla siku za mwisho hazijafika kwahiyo hutilii maanani sana kuhusu kuokoka na kuenenda katika maisha matakatifu, sasa hichi ni kitu kinachoweza kuonekana cha kawaida lakini sio cha kawaida, ni kama mtu akivaa shati na tai na koti vizuri alafu chini akavaa taulo akaenda hivyo mpaka kiwanja cha ndege mtoto wa miaka miwili ataona tu huyu mtu anataka kusafiri lakini kwa mtu mzima ataona hichi kitu si sawa si cha kawaida labda mtu huyo ana shida.
 
Jinsi unavyomchukulia Mungu ni tofauti sana, muda mwingine kama unaenda kanisani unaweza ukapita dukani ku change hela ili upate hela ndogondogo lakini hebu jiulize je ukienda sokoni huwa unapitia dukani ku change hela? au huwa unaenda na pesa yote?. Usipokuwa kiroho vizuri hutaweza kutofautisha kitu kilicho sawa na kisicho sawa, na usipooona kitu kisicho sawa hutaweza kubadilika, hutaweza kubadilisha mtazamo.
 
Usipo mruhusu Roho Mtakatifu akutawale hutaona kwamba ni kitu cha ajabu lakini utazani ni cha kawaida. Muda mwingine unaambiwa au unaonywa kabisa usifanye kitu flani lakini usipofunguka na kuona kweli ninakoelekea si kwa kawaida hutabadilika, na huwezi kubadilika mpaka uone unafanya vitu visivyo vya kawaida kama vitu vya kawaida, yule mwanampotezo baadae alijitambua na kugundua Luke 15:17-20, na muda mwingine unaweza kuona hichi kitu sio sawa lakini unahitaji uwezo/neema kutoka kwa Mungu ili uweze kuelewa, kwahiyo unaweza kuona kitu cha ajabu lakini usielewe. Sasa je unaona vitu visivyo vya kawaida? na kama umeviona je unachukua hatua gani? mwambie Mungu akupe ufahamu ili mambo yakitokea uelewe ni nini kinatokea na nini cha kufanya.

No comments:

Post a Comment