''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, June 21, 2015

UPENDO WA MUNGU

Mhubiri: Mch. Mainoya
Maandiko: Warumi 8:31-39, 2Wakoritho 11:26-27,12:10, Yeremia 31:3

Upendo wa Mungu ni mkuu sana unapita fahamu zetu, upendo wa Mungu sio kama upendo wa wanadamu, na upendo huo ndio unaoitwa upendo wa Agape. Mungu alitupenda wakati tupo dhambini, Yeye ndiye aliyetuchagua sisi akatupenda tukiwa na dhambi zetu, akaamua kumtoa mwana wake wa Pekee Yesu Kristo ili afe kwa ajili yako/yetu ndio maana hapa Paulo anasema nini kitatutenga na upendo wa Mungu?.

Mwanadamu atakupenda kwa sababu una kitu flani au kwasababu atapata kitu flani kutoka kwako, lakini Mungu alitupenda tu hatukuwa na kitu cha kumpa wala hatukuwa na kitu kizuri sana cha kumfanya Yeye atupende na kutuokoa bali alituokoa kwa neema tu, hatukustahili.  Mama aweza kumsahau motto wake mwenyewe lakini Mungu hawezi kutuacha.

Mungu anakupenda sana ndugu yangu na sio leo tu bali milele Yeremia 31:3, Upendo wa Mungu sio wa Muda fulani tu bali ni wa milele. Alimtoa Yesu kwasababu yetu basi ni jukumu lako wewe pia kumpenda na kumtumikia na kuishi maisha ya utakatifu ili ufike mbinguni. Uamuzi uko kwako sasa Mungu alishamtoa Yesu kwa ajili yako, Je unamkubali na kuishi katika utakatifu maisha yako yote? chukua hatua.

No comments:

Post a Comment