''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, June 15, 2015

KIUMBE KIPYA NDANI YA KANISA JIPYA

Mhubiri: Mr. Mwalongo
Maandiko: Warumi 6:1-10
 
Kristo Yesu baada ya kuleta ukombozi hapa duniani katika ile siku ya pentekoste kanisa jipya likazinduliwa, kwahiyo kanisa likaanza upya katika muundo mwingine kabisa na kanisasa hilo likaitwa kanisa la kipentekoste; na baada ya kuzinduliwa kanisa jipya kukawa hakuna namna mtu wa kale hawezi kuwa kwenye kanisa la kipentekoste, na ndio maana lazima uokoke kwanza lazima uzaliwe mara ya pili ili uweze kuwa katika kanisa jipya la kipentekoste.
 
Mtume Paulo alikuwa anazungumza na warumi kuhusu kuzaliwa mara ya pili anasema tufanye nini basi tutende dhambi kwasababu neema ipo, anazungumza kuhusu kuzaliwa mara ya pili, mtume Paulo haongelei habari za kurekebishwa kidogo yaani baada ya kuja kanisa jipya tunarekebishwa kidogo alafu tunaingia hapana!,sio kurekebishwa bali kuzaliwa mara ya pili ni habari ya kuwa kiumbe kipya na sio kurekebishwa. Kuingia katika kanisa hili lazima uzaliwe mara ya pili, na kuishi katika kanisa hili lazima uzaliwe mara ya pili hakuna namna nyingine, Mtume Paulo hakusema turekebishwe rekebishwe alafu tuingie kwenye kanisa hili. Mpango mzima wa Kristo Yesu sio kurekebishwa wala sio kutengenezwa bali ni kuzaliwa mara ya pili.
 
Tulivyokuwa hatujaokoka tulikua tuna asili ya dhambi, hata wakati mwingine ilikuwa ni rahisi kutukana, kusema uongo, kusengenya(kumsema mtu mwingine), kufanya uasherati au dhambi nyinginezo, na hata mwingine anasema mimi nashindwa kujizuia kufanya dhambi sasa katika hali hiyo ya kutekwa na dhambi kama utarekebishwa lazima utarudi tu! ni lazima uzaliwe mara ya pili ni lazima mtu/utu wa kale ufe na uzaliwe utu mpya ili uwe mtu mpya. Kwa jinsi mtu wa kale alivyo m-baya hafai ni lazima ukubali kuzaliwa upya katika roho.
 
Baada ya kuzaliwa mara ya pili yaani kuwa kiumbe kipya hutakiwi kurudia tena dhambi zako za kale, kiumbe kipya kitafanyaje dhambi? mtu wa kale alishakufa na maandiko yanasema ya kale yote yamepita na sasa umekua kiumbe kipya, ya kale yote yamepita na sio baadhi na sasa unatakiwa kuishi maisha matakatifu na ndio maana katika 1Petro 1:23 inaelezea kwamba uchafu wote, hila yote imeondoka na sasa umekuwa kiumbe kipya na kwa habari ya moyo unakuwa kama mtoto mchanga yaani hakuna baya ndani ya moyo wake hakuna kuwaza baya. Kiwang cha usafi wa moyo ni kama mtoto mchanga kwa habari ya matusi kwanza hata huyakumbuki yaani hata ukisikia mtu mwingine anayataja unatubu wewe, na huo ndio usafi wa kiwango cha kiumbe kipya.
 
 

 
 

No comments:

Post a Comment