1.YESU ALIONA MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUONA
2.YESU ALIAMINI MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUAMINI
3.YESU ALISEMA MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUSEMA WALA KUELEWA (spiritual language)
4.YESU ALISIKIA MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUSIKIA
5.YESU ALIFANYA MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUFANYA
JAMBO
LA KWANZA
YESU ALIONA MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUONA
1.
Yesu
aliwaona Makutano akawahurumia. Wengine waliona makutano na wakataka warudi
makwao.
Mathayo
9:36 “36 Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa
wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.”
Marko 6:36 “Uwaage
watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie
chakula.
Yesu anatutaka na sisi tuliomwamini tuone tofauti na dunia inavyoona.”
2.
Yesu
aliona senti ya mama mjane, wengine waliona mamilioni ya matajiri.
Marko 12: 41 – 42 “41 Naye akaketi kulielekea sanduku la hazina, akatazama jinsi
mkutano watiavyo mapesa katika sanduku. Matajiri wengi wakatia mengi. 42 Akaja mwanamke mmoja,
mjane, maskini, akatia senti mbili, kiasi cha nusu pesa. 43 Akawaita wanafunzi wake,
akawaambia, Amin, nawaambia, Huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote
wanaotia katika sanduku la hazina;”
Dunia huwaona wasio
nacho kama watu wa kupuuziwa na kuwekwa nyuma, Yesu huwaona watu wasionacho
kama watu wa muhimu na wakutangulizwa mbele.
3.
Yesu
aliiona nia ya ndani ya Zakayo, wengine waliyaona maovu ya Zakayo.
Luka
19:5 - 7
5 Na Yesu, alipofika mahali pale,
alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda
nyumbani mwako. 6 Akafanya haraka, akashuka,
akamkaribisha kwa furaha. 7 Hata watu walipoona, walinung'unika
wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi.
Yesu huangalia huyu ni nani kesho,
wanadamu huangalia huyu alikuwa nani jana.
·
Macho ya Yesu huangalia kuona maisha ya
kesho, bali macho ya wanadamu hunagalia kuona maisha yale ya jana.
·
Macho ya Bwana yanatafuta jema ndani ya
mtu, macho ya wanadamu yanatafuta maovu ndani ya mtu.
·
Macho ya Yesu yalimuona Paulo wa kesho,
wakati macho ya wanadamu yalimuona Sauli wa jana.
Paulo
wa kesho:
Matendo ya Mitume 9:11
Bwana
akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika
nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;
Sauli
wa Jana
Matendo ya Mitume 9:26 “Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao
walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi.”
4.
Yesu
aliona maelfu ya samaki na mikate, wengine waliona mikate mitano na samaki
wawili.
Mathayo
14:15 – 21
i.
Wanadamu waliona nyika iliyojaa ukame, Yesu aliona nyika iliyojaa neema, vyakula,
uponyaji wa mwili na roho.
ii.
Yesu alikuwa anaona mikate na samaki za
kula maelfu ya watu, wanafunzi walikuwa wanaona mikate na samaki za kula mtu
mmoja.
iii.
Yesu anataka uone kile anachokiona yeye
kila akiyaangalia maisha yako.
iv.
Kile anachokiona Yesu juu ya maisha yako
ni kikubwa sana kuliko kile unachokiona wewe katika uhalisia wake.
v.
Yesu anauona muujiza wako kabla
haujatungwa mim
vi.
Yeremia 1:5 “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni,
nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.”
5.
Yesu
alimuona binti wa Yairo akiwa amelala, wanadamu walimuona binti wa Yairo akiwa
amekufa.
Marko 5:35 - 43
i.
Watu walikuwa wakilia na kufanya
maombolezo makuu juu ya binti wa Yairo.
ii.
Wanadamu wanaokufanyia maombolezo juu ya
kushindwa kwako, wasubiri "suprise" ya Bwana Yesu.
iii.
Wanadamu walitangaza msiba wa binti
Yairo, Yesu alitangaza uzima wa binti Yairo.
Marko
5:39
iv.
Alipokwisha
kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali
amelala tu.
v.
Yesu hakusema msichana FUFUKA bali alisema msichana INUKA
Marko 5:41
41
Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana,
nakuambia, Inuka.
vi.
Wanaofikiri umekufa, waambie umeinama
tu, muda si mrefu utainuka.
6.
Wanadamu
wanakuona umebeba mimba, Mungu anakuona umebeba Mataifa. Mwanzo
25:21 - 23
i.
Rebeka aliona watoto wakishindana, Bwana
aliona mataifa yakishindana.
ii.
Wewe unaona umebeba nini? Umebeba mimba
au Umebeba Mataifa?
iii.
Mungu anataka uone kama anavyoona yeye.
No comments:
Post a Comment