Maandiko: Matendo 1:5-8
Mungu aliweka kanisa duniani kwa kusudi maalum, kwahiyo liko kusidi la Mungu katika kanisa na mmbeba kusudi hilo ni wewe. Mungu hakukuokoa ili uende tu kanisani ukae kwenye viti bali kwa kusudi maalum. Katika Matendo 1:4-8
"4 Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; 5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache. 6 Basi walipokutanika, wakamwuliza, wakisema, Je! Bwana, wakati huu ndipo unapowarudishia Israeli ufalme? 7 Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. 8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."
Maneno haya ni kati ya maneno ya mwisho kabla Yesu hajaondoka kwa maneno mengine tunaweza sema huo ni husia Yesu aliouacha kabla hajaondoka duniani. Hapo kuna mambo muhimu sana wanafunzi waliambiwa na Yesu. Na la kwanza; Wasitoke Yerusalemu na waingoje Ahadi ya Baba.
Paulo aliwaambia Wakoritho kwamba , roho inakaa ndani ya mwili alafu roho ndiye alishaye nafsi,ndio maana unapomuomba Mungu ili Mungu akusikie lazima uwe na toba sahihi kabla hujaanza kumwambia Mungu mahitaji yako. Lakini Mungu ni Roho, na mwanadamu amegawanyika katika sehemu tatu ;mwili, nafsi na roho, sasa pale unapotubu kwa kumaanisha Mungu anaingia kwenye roho na baadaye Roho anatia nguvu mwili, watu wengi wanaanguka katika uzinzi ni kwasababu mwili hauna nguvu ya kushinda tamaa, bali ukiwa na Roho wa Mungu, na baada ya hapo mwili utakubali ibada, utakubali kufunga.
Ushindi wa kanisa upo kwenye kujaa Nguvu za Mungu, Yesu aliwaambia wanafunzi "Lakini" lakini inaonyesha wanafunzi walikuwa na mashaka, wasi-wasi na kutoamini na hofu ya kwamba itakuwaje Yesu akiondoka.
No comments:
Post a Comment