''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Monday, May 9, 2016

NGUVU YA AGANO LA DAMU YA YESU

Mhubiri: Mch.Isack Edward Chalo
Maandiko: Mathayo 26:26-30

 Maneno haya aliyanena muda mchache kabla hajapelekwa msalabani, akachukua juisi ya mzabibu akawaambia hii ni damu ya Yesu ya agano.

Agano ni nini?
Turudi kidogo agano la kale, maana ya tangia wakati wa awali ni makubaliano au mkataba, ambao hufanyika kati ya mtu na mtu au na kundi au kudi na kundi. Kule mwanzo alifanya Mungu alifanya agano na wana wa israel lakini mwanzo alifanya agano na Ibrahim. 

Ibrahim aliaambiwa yeye na uzao wake wote, na chamzo cha hii ilikuwa anguko la binadamu kwahyo lazima kuwe na chanzo ambao ni wana wa israel na aliwaambia nyie mtakuwa na watu wangu. Waliwekwa kama shamba darasa ili watu wakiona jinsi ninavyoshughulika nanyi watu wengne waone kuwa yupo Mungu wa kweli.

 Kwahiyo kutokana na lile agano/ makubaliano wana wa Israel ilibidi waishi kwendana na yale makubaliano. Kutoka 24:1-8, wana wa Israel walielekezwa jinsi ya kuishi na mwishoni Musa akachukua damu akawapaka wana wa israel. Maagano lazima yawe na kitu cha nje cha kuashiria ndio maana walipakwa damu, kama makubaliano ya wana ndoa inavyotumika pete kuonyesha yale makubaliano. Sasa Mungu ili kuthibisha damu ya mnyama ilimwagika, na kipindi kile kulikuwa na maagano mengi tu lakini lilivyokuja agano la damu lilikuwa ni lenye nguvu na la hatari, lazima ukae chini ufikirie vizuri kabla hujaingia kwenye agano la damu, kwasababu damu inaonyesha uhai na hili agano si la mchezo ukilivuruga kwasababu lilichukua uhai wa kitu. 

Kwahiyo wana wa Israel baada ya agano ilibidi wajue jinsi ya kuishi kwasababu walikuwa tayari ndani ya agano. Kama sharti moja ni mtakuwa watakatifu kama mimi nilivyokuwa mtakatifu, 2. Watakuwa watumishi wake, 3. Watamheshimu Mungu mmoja tu, naye akasema mkifanya sehemu yenu nami nitafanya sehemu yangu, atawalinda na hilo analisema pia kwenye Isaya 43.  

Lakini wana wa Isreal walienda kinyume cha agano la Mungu na badae Mungu akaanza  kufanya agano na watu wote ambao wako tayari na damu itakayotumika kwenye agano hili jipya sio sawa na lile la kale. Agano hili jipya damu ya Yesu yenye dhamani kuliko zote ndio iliyotumika na sio kwa ajili ya wana wa Israel peke yake bali kwa mtu yeyote akimwamini Yesu na kukubali aingie kwenye maisha yake anaingia kwenye agano jipya.

Damu ya Yesu ya Agano Jipya ina kazi gani?
1. Inaonyesha kuwa ni kuna mkataba.
2. Ni kwa ajili ya ondoleo la dhambi
3. Ni kumkumbusha Mungu wajibu wake juu ya watu wale aliofanya nao agano la damu kama  kuwalinda na kuwaponya
4. Inanena mema juu ya masiha yetu.

INANENA MEMA GANI?
1. Inamkumbusha Mungu kuwa kuna watu wako duniani
2. Inamkumbusha juu ya mema yote kwa kila mtu mkristo aliyefanya agano na Mungu

Je Inanenaje Mema?
Kwa mfano kwa mtu analiyeambiwa na daktari ugonjwa anaoumwa hauwezi kupona, sasa ile damu inanena uponyaji juu yake, kwa mwanafunzi jambo jema ni kufaulu kupata ada na hapo pia Damu ya Yesu inanena mema, na kwa wafanya biashara jambo jema ni kupata mtaji, wateja waongezeke pia hata kwa hilo Damu ya Yesu inanena mema itatoa mtaji.



No comments:

Post a Comment