''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, June 19, 2016

ULINZI WA MUNGU KWA AJILI YA WATU WAKE

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Isaya 43:1-8
 
 
Utumwa ni kitu kibaya sana kilichowavamia wana wa israeli kwa miaka mingi sana. Hapa Bwana alimtumia nabii Isaya kuwatia watu hawa moyo wasiogope Mungu yupo nao na siku yao ya ukombozi imefika, wakati wao wa ukombozi umefika.

Mungu anasema Usiogope maana wewe ni wake, Mungu anakukumbusha leo kwamba usiogope kwa maana yuko pamoja nawe. Majaribu ni mito ambayo inaweza kukumba lakini Mungu anasema usiogope maana yeye yupo nawe.

Huu ndio unabii aliotoa nabii Isaya kwa ajili ya kuwatia moyo watu wa Mungu wa Taifa la Israeli.

Jina la Yesu lipo leo kukuinua toka katika matatizo na mateso ulio nayo sasa, mtumaini na mtukuza Yeye. maana Yeye atakuponya shida zako zote. Kwa miaka 70 taifa la Israeli lilikuwa katika utumwa lakini siku ya ukombozi ilipofika walikombolewa.

Mtukuze Bwana katikati ya magonjwa na matatizo yako naye atakuinua na kukutoa katika tabu na matatizo yako. Yupo  Yesu usilie mtu wa Mungu mtumaini Yeye na amini katika Yeye, nae atakuinua katika matatizo na mateso yako yote.

YESU NI BWANA YUPO KWA AJILI YAKO NAE ATAKUINUA NA KUKUPONYA KUTOKA KATIKA MATATIZO NA MATESO YAKO.
kwa imani mama aliyekua na msiba wa kutokwa na damu kwa miaka mingi aligusa vazi la Yesu na msiba wake ukakauka.
LEO NI SIKU YAKO YA KUPONA KUTOKA KATIKA MATATIZO NA MATESO ULIO NAYO...

No comments:

Post a Comment