''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, January 29, 2017

SHAUKU YA KUFANYA UINJILISTI AU KULETA WATU KWA YESU

Mhubiri: Samweli Lichali
Maandiko: Mathayo 28:19-20


Neno shauku ni neno la kawaida sana, shauku ni hali ya ndani au msukumo wa ndani wa kufanya kitu flani. Ukiwa na shauku ya kuleta watu kwa Yesu inamaanisha kwamba, utakuwa na msukumo kutoka ndani wa kumtangaza Yesu. Uinjilisti maaana yake ni tangaza habari njema.

Ndani ya injili kuna mambo makuu manne(4)
1. Yesu anaokoa
2. Yesu anatenda miujiza
3. Yesu anabatiza
4. Yesu atarudi tena 

Ndugu tambua kuwa Yesu ni kweli atarudi tena, kwahiyo katika mipango yako, weka mpango mzuri wa kuendelea kuwa mtakatifu ili uwe tayari kwenda na Yesu.

KWANINI UFANYE UINJILISTI
1.Ni agizo kuu, fanya injili sio kwasababu mchungaji au askofu ameagiza bali ni  kwasababu Mungu mwenyewe ameagiza. 

2.Idadi ya wenye dhambi ni wengi kuliko waliookoa, wanaozaliwa kimwili ni wengi kuliko wale wanaozaliwa kiroho, na injili ndio njia pekee ya kuwafanya watu wazaliwe upya kiroho.
3. Wenye dhambi wanakabiliwa na hali ya kupotea. Wenye dhambi wote wamepotea, mwenye dhambi amekufa hata kama anatembea maana ametengwa pamoja na Mungu, pia mwenye dhambi ni kipofu hata kama anatembea, ni gaidi wa kiroho kwasababu anapingana na Mungu, mwenye dhambi yoyote ni mdeni anadaiwa, mwenye dhambi yoyote ni mtumwa wa dhambi hata kama haionyeshi kiroho ni wafungwa kiroho hata kama anatembea kwa njema.
4. Ufanye uinjilisti kwasababu utadaiwa unapowaacha wenye dhambi kuendelea dhambini. 
5. Kuna taji imeweka iwapo utaleta mtu kwa Yesu.
6. Ujazo wa Roho Mtakatifu ulikuja ili kutusaidia kutangaza kazi ya Yesu. Kwahiyo kazi mojawapo wa Roho Mtakatifu ni kutupa ujasiri wa kutangaza habari njema za Yesu.

VIZUIZI VINAVYOFANYA WATU WASIFANYE UINJILISTI
1. Woga, acha kuwa muoga hutapoteza kazi, au masaomo kama ukihubiri injili.
2. Kuzani kuwa sio kazi yako kupeleka injili, hii ni kazi ya kila mwamini.

Shawishi watu kwa namna yoyote ili wampokee Yesu. Muda umefika amua leo kutangaza habari njema ya Yesu, anza hata kwa kushuhudia pale mtaani kwako.
Pokea nguvu za kuwaambia watu habari za Yesu.

No comments:

Post a Comment