''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, February 19, 2017

LINDA SANA MOYO WAKO

Mhubiri: Mch. Raphael Benjamini Achi
Maandiko: Mithali 4:23-27

Mungu alikuumba sehemu kuu mbili, Kichwa na Moyo. Ndomana kichwa akakiwekea cover gumu ambalo ni fuvu kwasababu ndiko akili iliko, na moyo pia ni wa muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Mithali 4:23 "Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima". 

Moyo ni kitu cha Muhimu sana kukilinda na kuwa nacho makini kwasababu muda mwingine unaweza kukudanganya mwenyewe; Yeremia 17:9 "Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?", Mwanzo 6:5-6 " 5 Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. 6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo". Sasa ili moyo wako uwe salama ni lazima ukubali kuishi na Mungu kwa kumaanisha. 

Elimu yako, cheo chako au fahari ya mali zako itakuwa ni bure kama moyo wako utakuwa umeharibika; Mathayo 15:8-9 " 8 Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. 9 Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu". Mathayo 7:20-23 " 20 Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. 21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, 22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. 23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi".

Daniel 14:28-37, Moyo ukiharibika haijalishi wewe ni nani hata kama ni profesa kama moyo umeharibika unaweza kufanya vitu vya ajabu, Mfalme Nebukadreza alikuwa ni mfalme mkubwa lakini hakutaka kumtukuza Mungu, akaanza kuwa na kiburi, mali alizopewa na Mungu akaanza kusema kuwa amezipata kwa sababu ya bidii yake, akamchukiza sana Mungu, Mungu akaamua kumpeleka akaishi porini. Huyu mfalme hakuharibika akili bali aliharibika moyo wake na kuanza kujivuna

Usijivune na akili uliyonayo, mali ulizonazo, uwezo ulio nao ni kwasababu Mungu amekupa. Ukianza kujivuna na kuwa na kiburi uje kifo cha roho yako kimekaribia, maana kifi cha roho kina hatua kuu SITA
  1. KIBURI huzalisha nguvu ya MAUTI
  2. MAUTI huzalisha nguvu ya UOVU
  3. UOVU huzalisha TAMAA
  4. TAMAA huzalisha DHAMBI
  5. DHAMBI huzalisha KIFO
  6. KIFO ni hatua ya mwisho.

Sasa Je ufanyeje?
Mruhusu Mungu auchunguze moyo wako; Yeremia 17:10 "Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake", Ezekiel 11:19 "Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama". Ukimruhusu Mungu atauondoa moyo wa jiwe na kukupa moyo utakao fuata maagizo yake.

Dawa ya kuutibu moyo ni Zaburi 119:9-11 "9 Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. 10 Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako. 11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi". Kwahiyo kubali Neno la Mungu ili moyo wako upone.

1 comment: