''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, February 26, 2017

KAA KATIKA UWEPO WA MUNGU

Mhubiri: Mr. Elisha Suku
Maandiko: Yohana 16:5-15, Warumi 8:26

Tangia mwanzo Mungu alipanga kuishi pamoja nasi, na ndio maana akamleta Yesu kuishi pamoja nasi na baada ya Yesu kuondoka hakutuacha yatima, akauendeleza mpango ule kwa kumtumia Roho Mtakatifu. Wanafunzi wa Yesu walisikitika wakati Yesu anawaaga lakini Yesu akawaambia wasisikitike kwasababu ni afadhali Yeye aende ili Msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu aweze kuja. Na badae pia aliwaambia kwamba wasitoke Yerusalemu mpaka watakapo pata Nguvu ya Roho Mtakatifu.

Kwahiyo wewe kama mtu uliyeokoka unapaswa kuwa na Roho Mtakatifu muda wote na Kukaa katika uwepo wa Mungu. Mungu alitaka uendelee kukaa katika uwepo wake ukiwa na Roho Mtakatifu, ili uweze kutambua na kuifanya kazi aliyokutuma hapa dunia. Bila uwepo wa Mungu hutaweza kutambua nini Mungu anataka ukifanye na jinsi ya kukifanya.

 Yohana 16:8 "Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu."
Huu mstari wa nane unaonyesha moja kwa moja kazi ya Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu atakuongoza kwenye kweli yote. Roho Mtakatifu ana kazi nyingi usiifunge akili yako kwamba Roho anafanya kazi fulani tu. Kama utajijengea tabia ya kumtegemea Roho Mtakatifu katika kila kitu unachikitenda, utafanikiwa sana katika maisha yako.

 Roho Mtakatifu anatupenda sana na anasikitika kweli mara nyingi unavyoamua vitu menyewe wakati Roho Mtakatifu ndio anayejua mpango huu ni mzuri au ni mbaya. Roho Mtakatifu anataka amiliki maisha yako asilimia yote na sio baadhi ya asilimia. 

Jiulize, Je bila hii nguvu ya Roho Mtakatifu utajuaje hatma yako?, utafukuzaje mapepo na nguvu za giza?. Kila mkristo lazima uwe na hamu ya Roho Mtakatifu.

No comments:

Post a Comment