''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Monday, March 6, 2017

WAJIBU WA MWANAMKE (WWK)

Mhubiri: Mrs. Daina
Maandiko: Isaya 41:8, Mwanzo 22:2-3, Yohana 15:14-15


Mwanamke ni nani?
-Mwanamke wa kwanza aliitwa hawa kwa maana kitu kizuri,ni kitu chororo cha kupendeza.

Utumishi wa WWK
Utumishi wa mwanamke wwk ulianzia marekani. Utumishi huu ni utumishi uliotukuka, kusudi lake ni 
1.kuletea familia baraka,
2.kuletea baraka wachungaji na familia zao,
3.kuletea baraka mitaa au eneo unaloishi,
4.kuletea Taifa baraka Yohana 15:14-15

 Utumishi huu ni wa urafiki na Mungu na wala si wa utumwa. Isaya 41:8,Mwanzo 22:2-3,
Fika mahali uone hakuna cha thamani katika ulimwengu huu wala chochote cha muhimu bali Mungu pekee na ukamtumikie kwa nguvu zako zote na akili zote.

 Tujihoji wenyewe kwamba:-
1. Ni jinsi gani tabia yako inamuumiza rafiki yako Yesu?
   Unamfurahisha rafiki yako?
2. Mwenendo wako unamfurahisha rafiki yako Yesu?
3. Maneno yako yanamfurahisha rafiki yako Yesu?
4. Utoaji wako unamfurahisha rafiki yako Yesu?

Utumishi wa kweli ni ule ambao unasema huwezi kumuumiza rafiki yako Yesu.

 MAMBO YA MUHIMU KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU
 1.Beba msalaba wako kila siku na mfuate Yesu
 2.Jaa Roho Mtakatifu na ukamtumikie Mungu

 KUMTUMIKIA MUNGU HAKUNA MAJUTO BALI KUNA BARAKA

No comments:

Post a Comment