''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, March 12, 2017

KUYAJUA NA KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU

Mhubiri: Mr. Frank Mwalongo
Maandiko: Mathayo 26:36-46, Luka 22:43-44

Hichi ni kipindi Yesu alichokuwa anakaribia kuteswa, aliwachukua baadhi ya wanafunzi wake kwenda kuomba. 

Katika Luka 26:39 "Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe".

Yesu anamuomba Baba yake lakini sio kama mapenzi yake apendavyo bali kama mapenzi ya Baba yake, tunaona Yesu aliweka mapenzi ya Mungu mbele kuliko mapenzi yake mwenyewe. Na mara ya pili katika sura hiyo Luka 26:42 "Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe". Yesu anaomba tena lakini kama mapenzi ya Mungu yatakavyo, Yesu hakuangalia vingine bali aliangalia mapenzi ya Mungu. 

Wakati ule alivyokuwa ndani ya mwili alikuwa anajua mateso na maumivu yatayo mpata kwahiyo alikuwa anaomba kama kikombe kile kama kuna uwezekano kimuepuke lakini si kwa mapenzi yake bali kwa mapenzi ya Mungu kwasababu alijali sana mapenzi ya Mungu. Yeu alikuwa yuko tayari kwa lolote ili tu mapenzi ya Mungu yatimie. Je na wewe leo upo tayari kwa lolote ili tu mapenzi ya Mungu yatimie?

Watu wengi wamekuwa wakipenda kufuata mapenzi yao na kuacha kusikiliza mapenzi ya Mungu. Sio kuhusu mapenzi yako, au nini unachotaka bali mapenzi ya Mungu, nini Mungu anachotaka ukifanye. Yesu hakuomba ili mwili wake unavyotaka kitokee bali alijikaza ili mapenzi ya Mungu yatimie.

Je, kila kitu unachofanya kuna mapenzi ya Mungu ndani yake?. Kuna mapenzi ya Mungu kwa kila jambo; badala ya kusema nataka kazi ile, au nataka kwenda kukaa sehemu fulani au nataka kuolowe na fulani; hebu jiulize Je Mungu anataka nifanye kazi wapi? na ipi?, anataka nikae wapi?, anataka niingie kwenye ndoa na nani? yawezekana unampenda mwingine tofauti na yule Mungu aliye kuongoza, sasa kama utafuata mapenzi yako badae utajuta na kupata matatizo ambayo usingeyapata kama ungetafuta kujua Mungu anasema nini na kufuata aliye/alicho kuelekeza.

Kuna upinzani mkubwa kati ya mapenzi yako na mapenzi ya Mungu; mfano ukipata pesa mapenzi yako yanasema usitoe pesa hiyo kwa Mungu lakini mapenzi ya Mungu yanakwambia toa fungu la kumi. Lakini kumbuka sio kuhusu mapenzi yako bali timiza mapenzi ya Mungu.

Ukijua mapenzi ya Mungu utafanikiwa sana kwenye maisha yako, Je nini mapenzi ya juu ya maisha yako?. Je unajua mapenzi ya Mungu kwako? Lakini huwezi kujua mapenzi ya Mungu kama huna mawasiliano mazuri na Mungu.

Zaburi 143:10 "Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa," Mfalme Daudi alimuomba Mungu amfundishe jinsi ya kufanya mapenzi yake, Na wewe leo Muombe Mungu akufundishe kufanya mapenzi yake.

No comments:

Post a Comment