''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, April 16, 2017

KUFUFUKA KWA YESU, NGUVU YA WOKOVU WETU

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel Mhini
Maandiko: Luka 16:1-8; 15-18

Wanawake wale walienda kuuangalia mwili wa Yesu kwasababu ilikuwa ndio desturi za Kiyahudi, lakini wakashangaa kaburi liko wazi Yesu hakuwepo tena alikuwa ameshafufuka. 

Yesu aliwaambia kabisa siku ya tatu atafufuka pia wakutane Galilaya, ndio walisikia lakini cha kushangaza siku ya tatu wakaenda kaburini. Kuwa na tabia ya kuamini Yesu anachosema, amini Neno la Mungu linavyokuelekeza. Yawezekana unakosa majibu yako au miujiza yako kwasababu ya ukosefu wa imani, huamini kile Yesu anachokwambia au anachokuahidi.

Luka 16:15-18 Yesu alipokaribia kuondoka, alituachia kazi ya kuwaleta watu kwa Yesu, Je umeshawaleta wangapi kwa Yesu?. Twende kila sehemu ya nchi tuwaambia watu kuhusu Yesu Mwokozi wa maisha yao. Na kila mtu atakaye mwamini, ishara zitamfata nao.No comments:

Post a Comment