''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Tuesday, April 11, 2017

DAMU YA YESU KRISTO

Mhubiri: Mr. Elisha Suku
Maandiko: Waebrania 9:11-22

Zamani wakati wa agano la kale, watu walitumia damu ya wanyama kufunika dhambi, kulikuwa hakuna njia ya kusafisha dhambi kabisa. Lakini Damu ya Yesu aliyomwaga kwa ajili yetu iliweza na inaweza kusafisha dhambi zote kabisa!.

Wakati wa mwanzo, Mungu alifanya agano la kwanza na wana-Israel lile agano la kale ambalo lilihusu sana mambo ya sheria japokuwa lilikuwa na mapungufu yake, lakini Yesu akaja akafa kwa jaili yetu akawa MPATANISHI kati yetu na Mungu na kwanzia hapo likafanyika agano jipya, ndani ya Yesu tukapata uwezo tena wa kuingia Patakatifu pa Patakatifu, sasa kwa kupitia Yesu tunaweza kuongea na Mungu moja kwa moja.

Faida ya Damu ya Yesu:

  1. Imetupa MSAMAHA wa dhambi, inasafisha dhambi zote kabisa.
  2. Ina uwezo wa KUSAFISHA akili zetu na nia zetu ili tumgeukie Mungu.
  3. Inatuweka HURU, Damu ya Yesu inatuweka huru mbali na utumwa wa dhambi.
  4. Imetuwezesha kuwa WARITHI wa Ufalme wa mbinguni.
  5. Inatupa AMANI, Damu ya Yesu inatunenea mema juu yetu.
  6. Inatupa UWEZO wa kushinda dhambi na uwezo wa kumshinda shetani.


No comments:

Post a Comment