''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, June 18, 2017

MAMBO MATATU MUHIMU KATIKA MAISHA

Mhubiri: Mch. Nelson Kazimoto
Maandiko: Ayubu 22:21

1. MJUE MUNGU ALIYEKUPA KUISHI
 Mungu aliyekupa kibali cha kuishi mpaka sasa, wakati unazaliwa wengine walikufa, wengine walipenda kufanya kazi kama wewe, kufanya biashara kama wewe, kuimba kama wewe lakini hawako hai, wewe Mungu amekuacha uko hai mpaka leo, mjue sana huyo Mungu aliye kuacha uishi.

Ayubu 22:21 "Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia."

Ayubu alikuwa tajiri sana lakini mali zake zote zikapotea gafla lakini hapa anasema mjue sana Mungu ili uwe na amani. Kwahiyo kumbe amani haitokani na mali nyingi bali inatokana na kumjua sana Mungu . Mjue sana Mungu ili uwe una amani. Haujaoa, haujajenga, una shida flani bali una amani wala haumlaumu Mungu una amani, kwanini? kwasababu unamjua Mungu na kwa hilo ameachilia amani kwako. Kama huna amani tafuta kumjua Mungu zaidi na zaidi.

 Hata kama unapitia changamoto  nyingi mno lakini Mungu akupe amani. Unaweza ukawa na mali nyingi pesa nyingi lakini kama huna amani hutazifaidi kitu. Unaweza pita kwenye pito ambalo mpaka wengine wanasema kama wao wangepitia pito lako wasingeweza lakini wewe unaona kawaida tu, ni kwasababu  ya Mungu tu.

Ayubu baada ya kupata amani anaendelea; 'ndivyo mema yatakavyokujia' mema yanakuja kwako. Mema sasa ndio maisha mazuri, pesa, magari. Ukimjua Yeye mema yatakuja. Kwanini mema yatakujia?  kwasababu kwanza umemjua Yeye. La kwanza kuliko yote ni KUMJUA MUNGU. Hata kama wachawi wanazuia hata kama wajipange vikosi na vikosi, Bwana Mungu atasambaratisha wote na mema yako yatakujia. Kila tatizo la mwanadamu nyuma yake kuna nguvu ya shetani sasa Bwana Yesu ataiondoa yote na mema yatakujia.

Unapomjua Mungu unakuwa na uwezo wa kuzikabili changamoto katika maisha, Mungu anakupatia uwezo wa tofauti wa kuzikabili changamoto katika maisha, wainuke wachawi majambazi unakuwa na uwezo wa kuwakabili. 

2kor 4:16-18, likija jaribu, liambie kwasababu ya Nguvu ya Mungu hulegei, Paulo anasema kwababu hiyo hatukubali kuonewa hatukubali kunyanyaswa, hata shetani akijiinua mwambie silegei. Kwenye jaribu/ mapito, huduma yako usilegee kwasababu Mungu amekupa uwezo. 

Mateso, magonjwa, shida isikuondolee amani, Kwenye Ayubu 42, Mungu akaukomesha uteka wa Ayubu!! Mungu huyu na akomeshe shida yako, mateso yako! Watu watakushangaa ni wewe au mwingine, ni wewe Bwana amekutendea, jana ulikuwa una hali mbaya lakini leo una hali nzuri. Waliokukataa watakurudia wewe.

2. KUWA MTU WA KUCHUKUA HATUA
Luka 5:1-11 Kuwa mtu wa kuchukua hatua, ukimjua Mungu, Mungu anakupa uwezo wa kuchukua hatu. Petro alihangaika usiku kucha bila kupata samaki, lakini Yesu alivyokuja ufukweni AKAKICHAGUA chombo cha Petro kati ya vyombo vingine, Yesu akamwambia twende kilindini Petro hakusema kitu wala hakusema tulikosa samaki lakini akachukua hatua ndipo badae akwambia hatukupata samaki lakini kwa neno lake Yesu atashusha nyavu na akapata samaki wengi sana. Kutoka kwenye hilo neno tunajifunza vitu viwili, Kwanza 'kuchaguliwa na Yesu kama Yesu alivyochagua kwenda kwenye chombo cha Petro', naomba Bwana achague chombo chako na badae akupe vitu zaidi. Na cha pili Petro alivyo chukua hatua  kwa kuamini lile Neno la Yesu, na wewe amua leo kuchukua hatua, usiangalie kwamba huko nyuma ulikosea mara ngapi baada ya kujaribu mara nyingi au usiangalie hali yako, wewe muamini Yesu chukua hatua!.

2Wafalme 7:3-16; wakoma wakachukua hatua hawakusubiri mpaka kufa bali walikuwa tayari na kuchukua hatua na badae Mungu akawatendea muujiza. Mungu atakuinulia watu watakao sababisha muujiza wako, wakoma wanne tu walivyo chukua hatua tu Mungu akafanya sauti kubwa mpaka jeshi la wafilisti likakimbia, wakoma wakapata chakula.

3. JIFUNZE KUKIRI USHINDI MUDA WOTE
Daudi alikiri ushindi alisema kwamba yeye ana uwezo wa kumpiga goliati, na hata goliati alipoanza kuja Daudi hakukimbia lakini aliendelea kwenda mbele kumkabili, usikimbie jaribu kabili jaribu, hakuna pepo litakalo simama mbele yako.

No comments:

Post a Comment