''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, April 22, 2018

KUOMBA KWA KUMAANISHA!

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: 1Wafalme 17:1-6,18:41-46

Elia alikuwa binadamu kama sisi/wewe akamuomba Mungu mvua isinyeshe na kweli haikunyesha na badae akaomba inyeshe ikanyesha. Somo letu leo litaangalia sana ule wakati anaomba mvua inyeshe.

Elia alikuwa anaomba kwa bidii na kwa kumaanisha tena bila kukata tamaa, na ndio maana alikuwa naomba alafu anamtuma mjakazi wake Elisha akaangalie nje kama kuna kitu kimetokea na kama bado anaomba tena, hakuacha tu na kukata tamaa kwasababu alikuwa na UHAKIKA NA MUNGU WAKE kwamba atatenda tu, kwahiyo akarudia kuomba vile mpaka mara ya saba (7) alipoona kawingu kadogo. Hakukata tamaa mpaka alivyoona kuna kitu kimetokea. Mpendwa ni mambo yapi ambayo umeyaombea mara kwa mara lakini hujapata majibu bado, usikate tamaa wala kuacha, endelea kuomba mpaka utakapopata jibu kwasababu Mungu wetu yupo na yu hai, hawezi kukuacha hivyo hivyo atakujibu tu kwa wakati wake.

Jambo jingine tunalojifunza kwa Elia ni ule uhakika katika alama ndogo sana ya jibu lake. Elia hakusubiri mpaka aone wingu kubwa limetanda ndio aamini sasa kweli mvua itakuja kubwa sana bali alivyoona kawingu kadogoo kama ngumu tena kwa mbalii, ilitosha kabisa kuwa na uhakika kwamba itakuja mvua kubwa. Je wewe unasubiri mpaka alama iwe kubwa ndio uamini kuwa Mungu amejibu maombi yako?

Ifike mahali uwe na uhakika na Mungu unayemwabudu, kuwa ni Mungu anayetupenda sana hawezi kukuacha hivi hivi, na ya kwamba anasikia maombi yetu na atajibu kwa wakati wake maana wakati wake ndio sahihi.

Ili ujibiwe maombi yako, ni lazima uzingatie mambo yafuatayo:
  1. Moyo safi
  2. Kuomba kwa kutumia Jina la Yesu
  3. Kumbuka kusamehe wenzako
  4. Kuomba kitu ambacho ni mapenzi ya Mungu
  5. Kushika maagizo ya Mungu na kuyatekeleza
  6. Kuwa na bidii ya kusoma Neno na kuomba mpaka kitu kitokee.
Mungu akubariki sana, uwe ni mtu wa kuomba kwa bidii na kwa kumaanisha.

No comments:

Post a Comment