Mhubiri: Dr. Philipo Sanga
Maandiko: Mwanzo 1:26-28
Mwanzo 1:26-28 "Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. 28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."
Mungu alikuumba wewe kwa mfano wake, alisema na tumfanye mtu kwa mfano wetu. Alivyosema kwa mfano wetu hakumaanisha ufanane nae sura(face) wala hakumaanisha mfanane huu mwili wa nyama, ndomana kila mtu ana sura ya tofauti na umbo la tofauti.
Aliposema tumfanye mtu kwa mfano wetu alimaanisha mtu huyo awe na hali ya Uungu ndani yake, kuwepo kwako wewe duniani kuwakilishe vile Mungu alivyo, wengine waone Mungu kupitia wewe. Lakini mwanadamu alipoasi alianza kupoteza ile hali na uwezo wa uungu ndani mwake mpaka Yesu alipokuja na kutukomboa, akatufanya tuwe wana wa Mungu, akaturudishia ile hali na uwezo wa uungu ndani mwetu, kwahiyo unapookoka unapata tena ile hali ya uungu ndani mwako.
Maandiko hayo juu (Mwanzo 1:26-28) yana maana pana sana na ya muhimu sana ambayo yamkini hukuwahi kuijua. Alivyosema tufanane nae aliweka na uwezo wa tofauti ndani mwetu na tabia za uungu.
Uwezo huo na tabia za Uungu ni kama zifuatazo:
- Alitupa uwezo wa KUTAWALA, Mwanzo 1:26, akasema wakatawale samaki wa baharini n.k, ndani mwako una uwezo una mamlaka ya kutawala kila kitu mpaka mamlaka ya kukemea nguvu zozote zinazoenda kinyume na Mungu. Wewe una uwezo wa kutawala.
- Akatupa uwezo wa KUZAA, hapa hakumaanisha kuzaa watoto tu bali alimaanisha kuwa mzalishaji "Productive", mtu wa Mungu popote ulipo kwenye kazi yako lazima uwe kweli mzalishaji ni lazima uwe ni mfano wa tofauti ofisini kwako hata usipokuwepo waseme angekuwepo mtu flani hii kazi ingeisha. Lazima uwe mzalishaji mwaminifu bila uvivu.
- Akatupa uwezo wa KUONGEZEKA (multiply), Huduma yako iwe inaongezeka, biashara yako iwe inaongezeka, kazi uwe unapandishwa vyeo hiyo ni sifa yetu shetani atakuletea vizuizi lakini lazima uing'ang'anie kwasababu wewe kufanikiwa ni asili yako.
- Alitupa uwezo wa KUTIISHA, tunatiisha kwasababu nguvu za Mungu ziko ndani mwetu, nguvu ya Mungu iliyo ndani mwako iondoe nguvu zote za giza utakapokuwepo, shetani asiweze kukaa kwa sababu ya utiisho ulionao.
No comments:
Post a Comment