UJUMBE WA LEO: USHINDI JANGWANI
(VICTORY IN THE WILDERNESS)
----------------------------------------------------------------------------------
MHUBIRI: PASTOR REV. EZEKIEL
MWAKAJWANGA
MAANDIKO: Mathayo 4:1-11
---------------------------------------------------------
Tunaona Roho alimpeleka Yesu
jangwani, hebu jiulize Kwanini Roho wa Mungu mwenye huruma na upendo alimpeleka
Yesu jangwani?, wakati jangwani ni sehemu ya shida?.Tambua ya kuwa kuna
uhusiano kati ya jangwa na ushindi, mtu wa Mungu huwa anapita kwenye vyote
yaani kwenye jangwa na ushindi, na fahamu kwamba jangwa na ushindi vinaenda
pamoja na jiandae kwa ushindi wako katika jangwa. Watakatifu wote waliofanikiwa
katika Biblia walipita jangwani, mfano Yusufu ambaye mwishoni alikuwa mwenye
cheo kikubwa sawa sawa na waziri mkuu lakini alipitia majaribu mengi kama
kuuzwa na ndugu zake kuwa mtumwa alipitia kuwekwa jela, lakini kote huko
hakumuacha Mungu hatimaye akashinda, ilimpasa apitie katika majaribu yale ili
baadaye apate kile cheo. Pia Yesu kabla hajaanza huduma Roho alimpeleka
jangwani maana huko ndo kwenye ushindi. Yesu alianza ushindi wake kule jangwani,
kila mkristo ana jangwa lake lakini wale wanaovumilia mpaka mwisho wataokoka, Ufunuo 2:10. Usitamani njia ya mkato
maana huko ndo kuna baraka ambazo sio za
kweli, pita njia iliyo sahihi ili upate mafanikio yatakayo mpa Mungu utukufu, Yakobo 1:2-4,12.
Kwahiyo ndugu yangu ili ufanikiwe sana ni
LAZIMA ukubali kupita jangwani maana huko ndo kwenye ushindi wako, maana huko
ndiko utakapojifunza kutembea vizuri na Mungu, kwahiyo furahia unapopita kwenye
majaribu maana ukitoka huko huwi tena mtu wa kawaida.
Amua sasa kukubali kuingia
jangwani lakini huku ukiwa na Roho Mtakatifu. Maana kuna majangwa/majaribu mengine
yasiyotoka kwa Mungu bali unajisababishia mwenyewe mfano unapofanya dhambi
mwenyewe au majaribu mengine ni mateso yanayosababishwa na shetani. Tambua ya kuwa
katika kila mafanikio shetani atakuwepo kukujaribu.
shetani alimwambia Yesu kwamba
ajitupe kwakuwa malaika watamchukua lakini Yesu kwa kujua Yeye ni nani na Mungu
ni nani akamjibu shetani imeandikwa usimjaribu Bwana Mungu wako. Watu
waliookoka wengi sasa kwa kutokujua wao ni Nanina Mungu wanaomwabudu ni nani
hasa wanaachilia haki zao bila kujua. Ni kweli hilo andiko la malaika
watakuchukua usije ukajikwaa lipo katika Zaburi
91:11 lakini halikusema utakapojitupa mwenyewe. Kuwa makini sana shetani
huwa anatabia ya kutumia maneno ya Mungu wakati usiopasa ili kukujaribu. shetani
alitaka kumpa Yesu ushindi kwa style anayotaka yeye, si kila kitu au kila muujiza au kinachofanya kazi
ni cha ki-Mungu. Mathayo 7:21-23.
Kuwa makini sana shetani ni
mjanja, alimwonyesha Yesu milki yote akamwambia atampa vyote kama akimsujudia
akawahau kwamba Yesu ndio aliyeviumba hivyo vitu na dunia nzima. Ndugu yangu
mwabudu Mungu peke yake tu, hata kama unapitia katika mambo magumu kiasi gani
usitafute njia ya mkato, kuwa mwaminifu unapokuwa jangwani.
Unapokuwa jangwani/katika majaribu kumbuka msaada upo karibu, unaweza ukaona kimya lakini kumbuka mwisho ndiko kuzuri vumilia, Yesu baada ya kumaliza majaribu Malaika walikuja kumtumikia, Yusufu baada ya lumaliza majaribu mwisho alikuwa waziri mkuu. Usikate tama mwisho ndo kuzuri.
No comments:
Post a Comment