''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, March 20, 2016

AMBATANA NA MUNGU

Mhubiri: Mr. Leandri Kinabo
Maandiko: Waamuzi 7:1-8
 
Kuambatana na Mungu au kushikamana na Mungu ni kuishi na kutekeleza maagizo ya Mungu kwa ukamilifu. Mara nyingi watu wengi wanashikamana na dunia na kuacha kushikamana na Mungu. Mungu alivyomuita Abrahamu alimtoa kule nyumbani kwao ili amtenge na mazingira yale, katika hii dunia ili uweze kuendelea kiroho na kushikamana na Mungu lazima UKUBALI kujitenga na mazingira yote yatakayoweza kusababisha wewe kurudi nyuma kiroho. Ukiokoka tu ndani mwako utaanza kuhisi kwamba mazingira fulani hutakiwi kuwepo basi itii ile sauti ya ndani .
 
Hatupaswi kushikamana na dunia kabisa ndiyo maana kwenye Warumi 12:2 Inatukumbusha kwamba hutakiwi kushikamana na namna ya dunia hii, usiifwatishe namna ya dunia hii bali tugeuzwe nia zetu.
 
Gideoni kama mwanadamu hakujua ni jinsi gani atawaokoa wana wa Israeli kutoka kwenye mikono ya wamidiani lakini kwasababu maisha yake yalikuwa yameambatana na Mungu, Mungu akamtokea na kumuelekeza jinsi ya atakaloenda nalo. Kuna faida nyingi sana utapata kama utaamua kuishi maisha matakatifu na kushikamana na Mungu.
 
Baadae Gideoni alianza kujiuliza tena itakuwaje kwasababu Mungu aliendelea kupunguza jeshi mpaka watu 300 kati ya watu 32,000. Akili Mungu zi juu sana na ana njia za tofauti kabisa za kukushindia shida zako. Kwasababu Mungu hafanyi kama wanadamu tunavyofanya vitu vyetu Mungu ana namna yake ya kufanya vitu.
 
Ukiwa umeambatana na Yesu hutakiwi kutegemea ni kiasi gani cha hela ili  uweze kutatua shida zako, hutakiwi kuhesabu jeshi ili ujue ni jinsi gani utashinda kwasababu hushindi kwasababu ya jeshi kubwa au kwasababu unatoa sana sadaka au una nguvu sana bali ni kwa neema tu.
 
Maswali ya Kujiuliza
1. Je una mwamini Mungu?,
2. Je unamtegemea Mungu asilimia 100?
 
Yawezekana unapitia hali tofauti tofauti lakini kama ukiwa pamoja na Yesu utafanikiwa.
 
Mambo ya Kuzingatia
1. Lazima utafute kuenenda kama Yesu atakavyo.
2. Mungu yupo tayari lakini ni lazima tufanye jukumu letu tusome Neno la Mungu, tuombe, lazima tuishi maisha matakatifu, Mungu alimwambia Gideoni atawaokoka lakini alimwambia cha kufanya, walitakiwa kwenda kwenye vita na kupiga tarumbeta.

3.Lazima umuweke Mungu wa kwanza, ukipata matatizo mwambie Mungu kwanza, hakuna siku mbili ambazo ziko sawa kila siku ni ya aina yake kwahiyo kila siku lazima umuweke Mungu kuwa wa kwanza.
4. Lazima uvae silaha zote za kiroho muda wote ili uweze kushinda vita vya kiroho.
5. Lazima uwe mtakatifu, na ukiwa mtakatifu Roho atakupa ujasiri, lazima kila siku ujikabithi na kuambatana na Yesu.
 
Kama unataka kuambatana na Yesu lazima umwamini Yesu Pekee yake na kumtegemea Yesu 100% hata kama ukipitia katika hali nguvu kiasi gani. Mungu anafanya kazi na watu wachache AMBAO WAKO TAYARI KUMTUMIKIA, Mungu anataka kufanya kazi na wewe lakini JE UKO TAYARI? lazima ujikane mwenyewe.

3 comments:

  1. Bwana Yesu asifiwe sana!
    Naifuraiya sana maneno ya Mungu. Inanipa mwangaza wa maisha ya utakatifu.
    Mungu anisaidie, ni chukuwe maneno katika blog hii, ili ni ifanye kuwa wimbo wa choir.
    Neema ya Mungu, iwe nanyi.

    ReplyDelete
  2. Mungu wa mbinguni akubariki sana
    Kwa somo nzuri
    Kwakweli nimepata kitu ndani yake
    Nimejifunza kupitia hili

    ReplyDelete