''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Monday, March 11, 2013

UJUMBE WA LEO: KUHESHIMU UCHAGUZI/ UMUHIMU WA WEWE KUCHAGUA
-----------------------------------------------------------------------------------------
MHUBIRI: MRS. MASEMBO
--------------------------------

Uchaguzi kwa hali ya kawaida una nguvu sana, nguvu hiyo inaweza ikawa nzuri au mbaya. Ukichagua vibaya utapata majuto makubwa sana lakini ukichagua vizuri utapata raha.
Aina  3 za uchaguzi:
1.  Uchaguzi wa Mungu kwetu, Waefeso 1:3-5
Mungu alitangulia kutuchagua sisi wakati tu wenye dhambi. Japokuwa tuliasi lakini Mungu alituchagua tuwe watoto wake kwa kupitia Yesu Kristo. Lakini Yesu hakutuchagua ili tukae tu bali alituchagua ili tumzalie matunda, na hayo matunda yapate kukaa.

2.  Jinsi Mungu alivyotuchagulia vitu
Muda wote Mungu anakuchagulia kitu kilicho bora. Mungu anatupenda sana kwahiyo hawezi kukuchagulia  vitu ambavyo sio vizuri. Na unapo pokea kitu kutoka kwa Bwana kitunze na kama ni huduma chochea zaidi na zaidi.

3.  Kuchagua wewe mwenyewe, Kumb 30:19-20
Leo umewekewa mbele yako uzima na mauti, kazi ni kwako kuchagua kimoja, chagua hivi leo ni yupi utakayemtumikia Joshua 24:15. Mke wa lutu alichagua kugeuka nyuma akawa jiwe la chumvi. Ni lazima uchague wewe binafsi. Na kila uchaguzi una gharama yake unaweza ukakuletea faida au hasara. Uchaguzi wako binafsi ni wa muhimu sana katika maisha yako mwenyewe kwasababu ukikosea utapotea. Esau alichagua kuuachilia uruthi wa uzaliwa wa kwanza kwasababu ya chakula cha dengu matokeo yake akakosa baraka. Chagua kutenda haki ili upate baraka, Ruth alichagua Mungu wa kweli na akabarikiwa.

No comments:

Post a Comment