UJUMBE WA LEO: MUNGU ANAWEZA KUONDOA UCHUNGU WAKO
-----------------------------------------------------------------------------
MAANDIKO YA SOMO:
1Samwel 1:1-23
MHUBIRI: MCH. MRS MAINOYA
----------------------------------------------
----------------------------------------------
Katika nyumba ya Elikana, kulitokea shida na hiyo shida
Eilkana kama mwenye nyumba alishindwa kuitatua, Penina ambaye alikuwa ni mke wa
pili wa Elikana alikuwa akiendelea kumchokoza Hannah ambaye alikuwa mke wa kwanza .
Hannah alipata uchungu mwingi, akaazimia na kuamua moyoni mwake ya kwamba ataenda Hekaluni kumlilia Mungu wake. Je! Nani leo ni penina wako? Je! Ni boss wako?, Je! Ni mume au mke wako?, Je! Ni nini kinachokusababishia uchungu?
Peleka shida yako kwa Bwana leo na uielezee vizuri kwa Mungu kwamba unahitaji nini hasa kama Hanna alivyosema anahitaji mtoto wa kiume. Pia tunaona hanna aliweka nadhili kwa Bwana, kuweka nadhili sio vibaya lakini cha muhimu ni kukumbuka nadhili uliyoweka, kama hanna alivyokumbuka kumtoa mtoto wake kwa Mungu alimpeleka mtoto wake kukaa kule hekaluni kwasababu alimuahidi hivyo Mungu.
Pia ukiomba amini hapohapo kwamba ulichoomba kimetendeka, hanna alipomaliza kuomba aliamini hapo hapo wala hakuweka shaka lolote. Usiogope aminin tu, inawezekana upo katika hali ngumu lakini amini tu, inawezekana huna kazi, huna mtoto, hupandishwi cheo, au biashara haileti faida au hitaji lolote lile wewe amini tu Mungu yupo kwaajili yako na anaweza yote wala usikate tamaa. Hatimaye Mungu atakupa kitu chema, Mungu hutoa vitu vyema tu, Hanna aliendelea kuamini hakukata tamaa baadaye alipata mtoto mwema ambaye ni Samweli ndiye aliyempaka mafuta mfalme wa Israel.
Kwahiyo hali unayopitia isikupe shida, Mungu ana kusudi na kila hali unayopitia katika maisha yako, cha muhimu ni kutokukata tamaa na kuendelea kumwamini Mungu na kutokumkufuru Mungu.
No comments:
Post a Comment