-----------------------------------------------------------------------------------
MAANDIKO: Mathayo 25:1-13
MHUBIRI: Mch. MHINI
---------------------------
Tunaishi wakati ambao uraia wetu
wa hapa duniani unaelekea ukingoni. Yesu anakuja kuchukua kanisa lake, kila
kitu chenye mwanzo kina mwisho ni kweli tumeshazoea kusikia siku za mwisho na
inawezekana unachukulia ni kitu cha kawaida lakini hii ni kama mchezo wa mpira
wa miguu baada ya dakika 90 refa akipiga pilimbi ya kumaliza, mpira unaisha
haijalishi umepata hujapata goli hata moja au umepata magoli mpira utaisha. Kipindi
tulichonacho sasa ni kipindi cha mwisho zaidi ya mwisho Yesu anarudi muda
wowote kwanzia sasa na akirudi haitajalisha umetubu au hujatubu historia
yamaisha yako itakuwa imeishia hapo na utatakiwa kusimama mbele ya kiti cha
hukumu, ni heri leo uamue kuishi maisha matakatifu yasiyo na mawaa.
Neno la leo linaonyesha wenye
busara watano walio weka mafuta ya akiba na wapumbavu watano ambao hawakuweka
akiba ya mafuta. Je! Una mafuta ya akiba? Mafuta ni uaminifu, Je! Umeambatana na
Roho Mtakatifu?
Ishara zote za siku za mwisho zinaonekana wazi
sasa, kama sunami, vimbunga vya hurricanes, njaa, vita katika nchi mbalimbali,
pia roho chafu kutoka kuzimu zimesambaa sana uovu umekuwa nje nje. Mathayo
24:7-14,36,42,44 inaoshenya ishara mbalimbali na hayo yote yametokea sasa ni
kwa kiasi gani umejiandaa?
No comments:
Post a Comment