''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, December 1, 2019

SIKU YA KUWAPONGEZA WACHUNGAJI

Mhuburi: Mr. Godfrey Zayumba
Maandiko: Warumi 10:12-15

Kuwapongeza wachungaji/ watumishi wa Mungu ni kitu cha maana sana kwasababu wanajitaabisha usiku na mchana kwa ajili yetu, wameacha vyote wamekuja kufanya kazi ya Mungu. Katika wana wa Israeli, watumishi wa Mungu walitokea kwenye kabila la Lawi, na kabila hili halikupewa eneo kama uridhi kwasababu wao maisha yao yalikuwa ni nyumbani kwa Bwana, ndivyo ilivyo hata leo, wachungaji hawafanyi kazi nyingine za kuajiriwa za kuingiza vipato, kwahiyo ni wajibu wetu kuwajali. Wachungaji wanafanya kazi kubwa sana, wewe unapata mafanikio katika kazi yako au biashara  zako ni kwasababu wachungaji wamekuombea, wachungaji wanakuombea mchana na usiku. Kuongoza kanisa lenye watu tofauti na wenye mitazamo tofauti si kazi ndogo bali ni kazi kubwa, wachungaji wanasuluhisha kesi nyingi, ni lazima tutambue kazi yao wanayoifanya na kuwapongeza.

Mambo muhimu ya kuyatambua kuhusu Mchungaji
1. Tuwatambue watumishi wa Mungu; ni lazima tutambue uwepo wao na kuuheshimu, lakini pia tutambue kazi kubwa wanayoifanya.
2. Wanatusimamia
3. Wanatuonya kwa Upendo kwasababu hawataki tuangamie wala umuache Yesu Kristo
4. Kuwastahi sana katika upendo- kumfichia aibu,tuwafichie aibu machungaji wetu, Haruni na Miriam walimsema Mussa gafla miriam akapata ukoma!
5. Kuwakumbuka, ni lazima uwakumbuke mchungaji wako kwenye maombi yako.
6. Wanatuongoza ili twende kwa usahihi
7. Wanatuambia Neno la Bwana, kila siku wanaanda chakula/Neno la Mungu ili upate malisho yaliyo bora 
8. Kuuwatii kwenye kile ambacho wanatuongoza
9. Kuwanyenyekea

No comments:

Post a Comment