''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Tuesday, January 28, 2020

KIU YA KWELI ILETAYO MABADILIKO

Mhubiri: Mrs. Lucy Masembo
Maandiko: Yohana 4:1-26

Yohana 4:7-15
7 Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe 8 Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula. 9 Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.) 10 Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai. 11 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai? 12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? 13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; 14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. 15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka.


Kiu ni shauku kubwa ya ndani ambayo mtu hawezi kutulia mpaka kile kitu kitimilike. Mwanamke Msamaria alikuwa na kiu ya kumjua Mungu zaidi na zaidi, Kiu ile ilimfanya ampokee Yesu, ilimfanya apate mabadiliko makubwa na baada ya hapo akawa kiumbe kipya, akaanza kuwa muinjilisti akaenda kuwaambia mji wote kuhusu Yesu.

Kiu au shauku ya kumjua Yesu inaleta mabadiliko. Shauku ndani mwako ya kumjua Yesu zaidi na zaidi itakuletea mabadiliko. Yesu Kristo akiingia rohoni mwako maisha yako hayawezi kubaki vile vile ni lazima yatakuwa na mabadiliko, kwa mfano utapata uwezo wa kushinda dhambi. Jawa na shauku ya kumjua Yesu zaidi na zaidi hutabaki kama ulivyo.

Kwanini sasa uwe na Kiu/ Shauku? Kwasababu
1. Kiu itakupa nguvu nyingine ya kutumika kwa ajili ya Mungu, ukikutana na nguvu ya Mungu utapata nguvu mpya ya kumtumikia. Kiu itakupa bidii ya kutumika kwajili ya Mungu.
2. Kiu italeta kutokujihurumia, ukijua Mungu aliyekuita ndani utafanya tu kazi yake.
3. Kiu itafanya kutokuogopa vizuizi  ambavyo vinaweza kutokea
4. Ukiwa na kiu hii inakupa shauku ya kumchagua Yesu kwanza, utaona Yesu kwanza na ndio mambo mengine.

No comments:

Post a Comment