''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, February 2, 2020

MKRISTO WA KWELI

Mhubiri: Mch. Kiongozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Matendo 5:1-11

Mkristo wa kweli ni yule anayeishi maisha matakatifu yanayompendeza Mungu na kuzingatia tunda la Roho. Ni yule anayesoma Neno la Mungu na kuliiishi, ni yule anayedumu katika kuomba.

Matendo 5:1-11
 "1 Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, 2 akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. 3 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? 4 Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. 5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. 6 Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika. 7 Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea.8 Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. 9 Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. 10 Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe."


Anania na mke wake Safira walipanga kumdanganya Roho Mtakatifu lakini Mungu hadanganyiki, Mungu anatisha akawaua hapo hapo. Amua Leo kuwa mkristo wa Kweli, hii ni January amua kupanga kusoma Biblia kwa mpangilio kama kwa sura, amua kuwa na mpango mzuri wa maombi, amua kuongeza viwango vyako kwa kumpenda Mungu, uzembe ulioufanya mwaka jana katika kumpenda Mungu usiurudie na mwaka huu. Dumu katika uaminifu ukimpenda Mungu siku zote.

No comments:

Post a Comment