''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Monday, November 25, 2019

KUWA MKRISTO WA KWELI

Mhubiri: Mch. Kiongiozi Abdiel M. Mhini
Maandiko: Luka 14:25-33, 1Petro 2:20-24

Kuwa Mkristo wa Kweli ni kumfuata Kristo kwa vitendo, kuishi kama Kristo alivyoishi, Yesu Kristo alivyokuwa hapa duniani aliishi maisha matakatifu ya hakutenda haki. Ndugu yangu kumfuata Yesu Kristo ni lazima uwe tayari kulipa gharama, kumfuata Yesu ni lazima uwe tayari kupambana na shetani na changamoto zote zitakazokuja mbele yako. Tangu siku unapookoka unakuwa umetangaza vita na shetani. 

Katika Neno tulilosoma, Biblia haisemi uwachukie wazazi wako lakini imemaanisha wazazi au ndugu zako wasiwe kizuizi cha wewe kuacha kumpenda Yeye, hata kama wote wakakutenga Yesu kristo atakusaidia na kukutunza. Utayari wa kuanza yote kwa ajili ya Yesu, hata kama kazi inaingiza pesa nyingi ikiwa inamuuzi Yesu achana nayo, afadhali ukose hiyo hela isiyo na haki ukamfuata Yesu. Kuishi maisha ya Kikristo ni kumfanya Yesu Kristo awe namba moja kwako, achana na vitu vyote vinavyozuia uhusiano wako na Mungu. 

Ndio labda umeshampokea Yesu lakini Je mpaka sasa umekuwa mKristo wa kweli, maisha yako yamefanana na Kristo? Je unamsikiliza Roho Mtakatifu?, Kuwa mkristo wa kweli ni kusikia Roho Mtakatifu na kufanya anayokuongoza hata kama halitawafurahisha watu wanaokuzungu ilimradi ni cha haki na ni mapenzi ya Mungu inabidi ukifanye. 

Lazima uwe mvumilivu, kama kweli unataka uwe mwanafunzi wa Yesu ni lazima ujikane mwenyewe kuna baadhi ya vitu kwasababu umeokoka hutatakiwa kuvifanya.

Matatizo ya kifamilia yasikuzuie kuwa Mkristo wa kweli, Luka 14:26. Mali za hapa duniani hazitakiwi kukuzuia kumfuata Yesu, Mathayo 19:20-24. Ubarikiwe!

1 comment: