''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, November 17, 2019

YESU KRISTO BADO ANATENDA HATA SASA

Maandiko: Waebrania 13:8 

Waebrania 13:8
"Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele."

Yesu Kristo yu Hai, bado anaishi bado anatenda miujiza bado anaweza kutenda mambo yaliyoshindikana kwa wanadamu. Mungu ni Yule Yule jana leo na hata milele, Yeye habadiliki, hazimii wala hachoki, aliyegawanya bahari ya shamu wana wa Israeli wakapita na kuua jeshi la farao ndiye Mungu hata leo, haijalishi unapitia hali ngumu kiasi gani, Mungu atakutoa kwenye hali hiyo, Yesu Kristo yupo kukusaidia. Yesu alisema katika Mathayo 11:28 "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha."

Haijalishi umeteseka kwa kiasi gani, njoo kwa Yesu atakupumzisha, hali ngumu unayopitia mwambie Yesu leo yuko tayari kukusaidia. Yeremia 32:27 "Tazama, mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza?" Je kuna jambo gumu la kumshinda Yesu Kristo? jibu ni Hakuna! kwahiyo ile shida yako kubwa kwako mwambie Yesu Kristo na umwamini naye atafanya!

Mathayo 7:7-8 "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; Kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa." Yesu Kristo anasema uombe nawe utapewa, mwambie Mungu mahitaji yako. Pia katika Hesabu 23:19 "Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?" Mungu ni Mungu sio kama mwanadamu anayetoa ahadi na kubadilika badae, Mungu hasemi uongo ahadi zake zote alizokuahidi zitatokea, amesema ukiomba utapata basi omba na uamini kwamba utapokea na kweli itatokea. Mungu akubariki sana.


No comments:

Post a Comment