''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, October 27, 2019

UTENDAJI WA MUNGU NYUMA YA MAMBO UNAYOPITIA (WORK OF GOD BEHIND THE SCENE)

Mhubiri: Mch. Isack Challo
Maandiko: Mwanzo 45:1-8, Mwanzo 15:12-16

Mwanzo 45:1-8
"Hapo Yusufu hakuweza kujizuia mbele yao wote waliosimama karibu naye. Akapiga kelele, na kusema, Mwondoeni kila mtu mbele yangu. Wala hakusimama mtu pamoja naye, Yusufu alipojitambulisha kwa nduguze. Akapaza sauti yake akalia, nao Wamisri wakasikia. Watu wa nyumba ya Farao nao wakasikia. Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ndimi Yusufu; baba yangu angali hai bado? Wala ndugu zake hawakuweza kumjibu, maana waliingiwa na hofu mbele yake. Yusufu akawaambia ndugu zake, Karibuni kwangu; basi, wakakaribia. Akasema, Mimi ni Yusufu, ndugu yenu, ambaye mliniuza kwenda Misri. Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna. Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi, na kuwaokoa ninyi kwa wokovu mkuu. Basi si ninyi mlionipeleka huku, ila Mungu; naye ameniweka kama baba kwa Farao, na bwana katika nyumba yake yote, na mtawala katika nchi yote ya Misri".


Huu ni moja ya ushuhuda mzuri sana wa jinsi Mungu anavyofanya kazi kwa njia ya tofauti mno zaidi ya vile tunavyodhani. Yusufu alivyokuwa mdogo aliota ndoto kwamba familia yao yaani baba na ndugu zake watamuinamia yeye na wakati yeye ndiye mtoto wa mwisho, na ndoto zile ziliendelea kaka zake wakata kumuua ili asiwasumbue na zile ndoto zake. Kwahiyo kaka za Yusufu walitaka kuiua ile ndoto wasijue kwamba Mungu anafanya kazi nyuma ya mambo unayopitia, wakamuuza kama mtumwa kwa wamisri wakizani kuwa watakuwa wamezuia ile ndoto, wasijue kwamba kwa kufanya vile wametengeneza daraja kwa Yusufu kwenda kwenye hatua nyingine zaidi.

Yawezekana na wewe leo unapitia hali ngumu unajiuliza kwanini mambo yanakuwa hivyo, kumbe kupitia shida hiyo ni daraja la kwenda hatua nyingine, maadai zako wanaweza wakadhani wamekumaliza kumbe wamekuwa ni sababu ya wewe kwenda hatua nyingine ya mafanikio yako.

Ukisoma Zab 105:7-19, utaona kwamba Yusufu alienda Misri akiwa amefungwa minyororo kama mtumwa akiwa katika maumivu hakujua nini kitatokea, lakini kumbe Mungu alikuwa anafanya kazi nyuma ya pazia, kumbe Mungu alikuwa naye hakumuacha. Katika hali ngumu muda mwingine ni vigumu kuamini kwamba Mungu bado yupo pamoja na wewe. Yusufu alienda Misri akiwa ni mtumwa mwenye maumivu kumbe ilikuwa ni mpango wa Mungu ili Neno lake litimie ili ile ndoto aliyoiota itimie.

Mipango ya Mungu katika maisha yako itatimia tu haijalishi watajitahidi kiasi gani kuzuia mafanikio yako, wakati wa Mungu ukifika kila kitanyamaza hakitaweza kuzuia kamwe. Kama una ombi ambalo bado Mungu hajalitenda, usikate tamaa, na umtegemee sana Roho Mtakatifu. Wakati wa Mungu ukifika! Umefika! hakuna atakayeweza kuzuia.

1 comment:

  1. Ninamshukuru sana Dk dawn acuna, aliandika uchawi wa mapenzi ambao ulimrudisha mpenzi wangu wa zamani katika masaa 48, shukrani kwake, ikiwa una hali kama hiyo.
    *Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
    *Kama unataka kupata mimba.
    *Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
    Ikiwa unataka kuponya aina yoyote ya ugonjwa. Na wengine,
    Wasiliana naye yeye ndiye mtu sahihi wa kutatua tatizo hili.
    Barua pepe: { dawnacuna314@gmail.com }
    Whatsapp: +2348032246310

    ReplyDelete