''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, October 20, 2019

UNYAKUO / KUJA MARA YA PILI KWA YESU KRISTO

Mhubiri: Mch. Isack Challo
Maandiko: 1Wathesalonike 4:13-18

1Wathesalonike 4:13-18
"Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo."


Hii ilikuwa ni waraka/barua ya Paulo kwa Wathesalonike, katika sura hii alikuwa anawajibu swali la muhimu lililokuwa linawatatiza sana kwamaana kulikuwa na mchanganyiko wa mafundisho ya nini kitafuata baada ya kufa na watu wakifa wanaenda wapi?

Mpendwa, habari ya Unyakuo na kuja kwa Yesu kwa mara ya pili ni ya kweli tena imekaribia sana sana. Watu wengi huwa wanachanganya kati ya Unyakuo na Kuja kwa mara ya pili kwa Yesu Kristo. Unyakuo ndio utakaoanza, utatokea kwa haraka sana ni zaidi ya kufumba na kufumbua, itatokea gafla sana, wale walio ndani ya Yesu watanyakuliwa, mtakuwa mpo wawili moja atanyakuliwa mmoja atabaki, baada ya hapo itakuja miaka 7 ambayo kwa waliobaki huku duniani dhiki kuu itaanza kwa wakati huo kwa wale watakatifu walionyakuliwa kazi zao zitakuwa zinapimwa na kupongezwa na kufutwa machozi kwa kazi walizofanya duniani, na baada ya miaka 7 ndipo Yesu atakapokuja duniani kwa mara ya pili, watu wote watamuona, Ufunuo 1:7.

Swali kubwa kwako Je, Yesu akurudi sasa hivi upo tayari? Muda umekaribia sana katika unyakuo na dalili kubwa ni mafundisho ya uongo yanayoendelea sasa hivi, unyakuo unaweza kutokea muda wowote, JE UPO TAYARI? nini cha kufanya ili kujiandaa ni kufanya kazi ya Mungu kwa bidii yote, kuishi maisha matakatifu muda wote kwasababu haijulikani ni lini unyakuo utatokea, kutakuwa hakuna muda wa kutubu, ni vizuri ukajianda sasa.

Kipindi cha dhiki kuu ni kipindi kibaya sana chenye mateso makubwa mno, na kuachwa na Yesu Kristo ndo kibaya zaidi, waliobaki duniani watateseka mno!

No comments:

Post a Comment