''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, October 13, 2019

WAPI UMEWEKA HAZINA ZAKO?

Mhubiri: Mzee wa Kanisa, Mr. Leandri Kinabo
Maandiko: Mathayo 6:19-21, Luka 12:13-20,Mithali 11:28, Mathayo 6:11, Mithayo 19:17-21

Mathayo 6:19-21
"Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako."

Luka 12:16-21
"Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu."


Hazina ni kitu cha thamani mtu unachokiweka kwa ajili ya baadaye. Kwa hapa duniani hazina inaweza kuwa ni pesa, madini n.k, lakini pia unaweza kuweka hazina zako mbinguni kwa njia nyingi kama kujitoa mwenyewe kufanya kazi ya Mungu au kutoa mali zako kwa ajili ya kazi ya Mungu. 

Kuweka hazina yako hapa duniani si kitu kibaya lakini tambua kwamba hapa duniani tunapita kuna maisha baada ya hapa duniani na huko ndipo tutakaa muda mrefu kuliko hapa, sasa je umejiandaaje? Je ni kwa kiasi gani umeweka hazina zako mbinguni?. Hata kama uwe na fedha kiasi gani ukifa utaziacha, je umeeandaaje huko utakapoenda? 

Hazina yako ilipo ndipo moyo wako utakapo kuwepo, je umeweka wapi hazina zako? weka akiba yako mbinguni mahali salama.

Ukiweka hazina zako mbinguni unaweza ukazitumia hazina hizo ukiwa bado hapa duniani, katika Isaya 38:1-6 Mfalme Hezekia alimkumbusha Mungu mambo aliyomfanyia na akapata kibali cha kuendelea kuishi. Tumia nguvu zako, pesa zako kuwekeza hazina zako mbinguni.

Njia unazoweka kuweka hazina mbinguni
1. Kwa kuwasaidia wahitaji, Mathayo 6:1-4
2. Kuwasaidia watu ambao hawawezi kukurudishia, Luka 14:13-14
3. Unaweza kuweka hazina kwa kufanya maombi, maombi yako yakakumbukwa
4. Kwa kumpenda adui yako, Mathayo 5:46-48
5. Kwa Kuvumilia majaribu unayopitia Mathayo 5:11, 2Tim 4:7-8
6. Kwa kumtumikia Mungu, unaweza kutoa hela, au kutoa nguvu zako muda wako, kama watu wanaoenda kuhubiri injili.

No comments:

Post a Comment