''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, October 6, 2019

NEEMA YA MUNGU YAKUTOSHA, ENDELEA MBELE!

Mhubiri: Mr. Victor Adrian
Maandiko: Kutoka 14:1-28

Hii ni safari ya wana wa Israeli kutoka Misri, katika safari hii Mungu aliruhusu changamoto nyingi, ilikuwa ni mpango wa Mungu kuwafundisha zaidi kuhusu Yeye lakini pia kuwasaidia. Ikumbukwe kwamba wana wa Israel walikuwa wamekaa katika utumwa zaidi ya miaka 400 kwahiyo kizazi kilicho kuwepo kwa wakati huo kilikuwa hakimjui vizuri Mungu wa kweli wa Israel yukoje na ukitaka kudhibitisha hilo ni pale walipoacha na Musa, Musa alivyopanda mlimani kuchukua amri kuu wana wa Israel walitengeneza mungu sanamu anayefanana na miungu ya Misri, kwahiyo inamaanisha walikuwa wanamwabudu Mungu wasiye mjua vizuri. 

Lakini pia kizazi hiki kilikuwa hakimjui Musa kwasababu Musa hakuwepo Misri zaidi ya miaka 40 kwahiyo kilikuwa ni kizazi kipya kisichomjua Musa, kwahiyo hata wao tu kukubali kwenda na Musa haikuwa kazi rahisi. Sasa hapo changamoto ya kwanza mbele kuna bahari kubwa hakuna njia na huku nyuma jeshi wa Misri linakuja ili liwakamate, ilikuwa ni hali ya kutisha, wana wa Israel wakapata woga wakasahau hata kuhusu Mungu wakaanza kumlaumu Musa kwanini aliwatoa Misri, yawezekana na wewe unapitia hali ambayo ukiangalia kila upande huoni njia ya kutokea, ukiangalia huoni njia ya m-badala, lakini Mungu anakwambia leo kwamba "Neema yangu yakutosha, Endelea Mbele!" hakuna kukata tamaa, Yesu uliyenaye ni Yesu Kristo mwenye nguvu kubwa sana anayeweza kufanya chochote kutoa njia kusikokuwa na njia, hata kama wanadamu wamesema haitawezekana kwa jinsi yoyote lakini kwa Mungu yote yanawezekana!


Mungu aliyewatoa wana wa Israel kule Misri ndio huyo huyo aliyefanya Farao atume jeshi lake kuwarudisha Misri wana wa Israeli, alifanya hivyo makusudi ili kupitia jambo hilo Mungu ajipatie Utukufu. Hapa tunajifunza kuwa mara nyingne unaweza kudhani changamoto unazopitia ni za kwako kumbe ni kwa ajili ya adui yako ili Mungu apate Utukufu kupitia hilo. 

Lakini pia Mungu anaweza kukupitisha kwenye changamoto nyingi ili kukuweka sawa, usilie tu, Mwamini Mungu kwamba anaweza kukutoa kwenye changamoto yoyote ile. Wana wa Israeli walipouona muujiza huu wa bahari kugawanyika walimuelewa Mungu kwa kiwango kingine. Usimuache Mungu kwasababu ya shida yoyote, Mungu anaweza kufanya kitu chochote, usikate tamaa, endelea Mbele!

No comments:

Post a Comment