''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Monday, September 30, 2019

ITUNZE NEEMA ULIYOPEWA

Luka 1:26-30
1Samweli 16:11

Luka 1:26-30
"Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu."


Neema ni nini?
Neema ni upendeleo anaopata mtu bila kuutabikia, neema ikiwepo kwa mtu kila kitu hukaa sawa, isipokuwepo hata ufanyaje mambo hayakai sawa.Neema ikwepo hata maadui zako wanakuwa hawakuwezi.

Kwanini unahitaji Neema? 
1. Kwasababu; neema inakupa upendeleo, neema ikiwepo hata kama adui wainuke vita iwepo, utapata tu upendeleo, haijalishi shetani atapanga majeshi kiasi gani Neema ya Yesu itakupa upendeleo.

2. Neema inatupa kushinda vita 1Samwel 17: Daud alienda kupeleka chakula vita akakuta askari wamemshindwa goliati, wakamwambia huyu humuwez lakini Daud kwasababu aliijua neema ya Mungu jinsi inavyofanya kazi, akampiga goliati.  Yawezekana na wewe ukawa unapitia vita vikali na unajiuliza utashinda vipi, nakwambia unahitaji Neema ya Mungu.

3. Neema inatukutanisha na fursa, wako wengi wanakimbizana huku na kule wanatafut fursa lakini hawapati, lakini jibu ni Neema ya Mungu, Neema ya Mungu ilimkutanisha Daud na kiti cha mfalme. 

No comments:

Post a Comment