MAANDIKO: Yeremia 17:5-8
MHUBIRI: Mrs. Subira Mitimingi(Mama Mch. Mitimingi)
Yeremia 17:5-8; “5. Bwana
asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa
kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. 6 Maana atakuwa kama fukara
nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika
nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana,
Ambaye Bwana ni tumaini lake.
8 Maana atakuwa kama
mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu
wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka
wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.”
Biblia inaweka wazi kuwa anayemtegemea mwanadamu amelaaniwa,
kwahiyo tambua kwamba ukimtegemea mwanadamu tu utakuwa umejipatia laana papo
hapo. Amua leo kumtegemea Mungu na kumfanya awe kinga yako. Mungu si kama
mwanadamu, mwanadamu ni kigeugeu, mwanadamu ana kikomo.
Kwahiyo usikubali ngugu yangu kutegemea mwanadamu kwasababu
utakuwa unatembea na laana.Mungu hampendi mtu anayemtegemea mwanadamu,
ukimpenda mwanadamu Mungu anajitoa ndani mwako anakaa pembeni. Lakini tambua
kuwa Mungu akijitoa katika maisha yako, ulinzi wa maisha yako utaondoka kwahiyo
shetani atapata nafasi ya kukutesa kadiri anavyotaka.
Siku za leo, kuna baadhi ya watu wanaamini kwamba uponyaji
unapatikana katika kanisa flani au kwa mchungaji flani au mchungaji flani
akikuombea ndo utapona au mpaka uende kuombewa kanisa flani ndo utapona,
Nakutaarifu kuwa hutapona wala hutapata Baraka wala mafanikio kwa njia hiyo
bali utajiongezea laana kwasababu huko ni kumtegemea mwanadamu kuliko Mungu au
huko ndo kulitegemea kanisa flani kuliko Mungu, na Biblia inasema amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye mwanadamu,
kwahiyo utakuwa umelaaniwa papo hapo. Ndugu yangu amua leo kumtegemea Mungu
tu!.
Pia, ukimtegemea mwanadamu Mungu huondoa hazina yake iliyo
ndani mwako, mfano kama ulikuwa ni mwimbaji mzuri karama ile ya uimbaji
itaondoka na utaanza kuimba vibaya.
Ukimtegemea mwanadamu utakuwa unakaribisha roho ya ufukara
katika maisha yako(angalia mstari wa 6)
Hata siku moja usiseme bila flani mimi siwezi kufanya kitu
flani, mfano mtu aliye na huduma asiseme bila mtu flani huduma hii haitaweza
endelea au bila flani huduma hii isingekuwepo, eti kwasababu anachangia pesa
nyingi au kwa kiasi kukumbwa. Kama utasema hivyo ipo siku Mungu atamtowesha mbali
huyo mtu anayechangia sana ili upate shida umkumbuke Yeye.
Ukimtegemea mwanadamu, utakuwa na maisha ya uchungu
kwasababu Baraka za Mungu zitaondoka
hazitakufuata.
Ndugu yangu tambua hili, Baraka za Mungu zinatakiwa ziwe
zinakufuata na sio wewe uzifuate. Watu wengi sasa wanahangaika huku na kule kisa
wanatafuta Baraka/ kubarikiwa, kwa njia hiyo ndugu hutapata Baraka za kweli,
Tenda haki Baraka zitakufuata popote ulipo, Yeremia 17:8.
Mfalme Suleimani alimtegemea Mungu akapata Hekima ya Ki-Mungu,
Mfalme Daudi pia alimtegemea Mungu akaweza kumuua goliati kwa kajiwe kadogo. Kwahiyo
siri kubwa ni kumng’ang’ania Mungu tu.
Vitu vyako vingi haviendi kwasababu unategemea akili zako
mwenyewe au unamtegemea mwanadamu mwenzako. Amua leo kumtegemea Mungu acha
kujitegemea, kutegemea pesa au mwanadamu.
No comments:
Post a Comment