''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, October 13, 2013

WATAKATIFU TUWE NA UMOJA



MHUBIRI: Mrs. Neema Mumghamba
MAANDIKO: 2Koritho 1:3-4, Yohana 17:11-22
Watakatifu tuwe na umoja. Bwana Yesu alipokaribia kuondoka, aliomba kwa Baba yake aliyemtuma, kwamba tuwe na umoja kama Mungu alivyo ndani ya Yesu na Yesu ndani ya Mungu.

 Tumeona mfano wa umoja katika msiba wa Dora uliotokea, watu walishirikiana kwa hali na mali na kufanya kazi kwa bidii na kwa kujitolea kutoka mioyoni mwao. Kuna siri ya umoja katika Mungu aliye Hai, Tunamuona Mungu alivyo mzuri katika umoja. 

Hebu tupende kumpa nafasi huyu Mungu, hebu tumsikilize, tufanye anayotaka, changamka sasa mtu wa Mungu, umoja ambayo yesu aliuomba ni kwamba Mungu awe ndani yetu na sisi ndani yake ili hata wanaotuzunguka walione hilo, waone maisha yetu ya tofauti, na wajifunze kutoka kwetu. Yamkini umemzoea sana Yesu siku hizi lakini inatakiwa watu waone kwamba kweli Yesu yupo ndani yako ndani ya  maisha yako, kwenye kazi yako aonekane, kupitia biashara yako ajulikane. 


Wanafunzi baada ya hapo wakahubiri injili kwa umoja, na sisi tupeleke injili na kulitangaza Jina la Yesu kwa umoja. Katika kitabu cha Yohana 15, kinaeleza kwamba, Yesu akikaa ndani mwako ukiomba lolote atakupa, tukae vizuri na Yesu, Mpe nafasi Mungu wako, Tuwe na Umoja kama Yesu alivyokuwa na umoja na Mungu baba. 

Paulo alisema tuwe na umoja katika kristo hakuna cha huyu ni myunani huyu ni myahudi wote tupendane na kuwa na umoja, Hebu tuwe na bidii na Yesu, sisi tuwe ndani ya Yesu na Yeye awe ndani yetu, basi tujifunze leo kama Bwana Yesu alivyoumba umoja nasi tuwe na umoja,amen

 

No comments:

Post a Comment