''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, November 17, 2013

IBADA YA LEO

UJUMBE: HAIWEZEKANI ISIPOKUWA KWA KUFUNGA NA KUOMBA
MAANDIKO: Mathayo 17:14-21
MHUBIRI: Mr. Frank Mwalongo

 Wanafunzi wa Yesu walimuombea yule kijana lakini lile pepo halikumtoka yule kijana, wanafunzi wake wakamfuata badae kwa faragha wakamuuliza kwanini hawakuweza kumtoa yule pepo, Yesu akawajibu kwenye mstari wa 20-21 "Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.21 Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga." Yesu yuko juu ya mapepo,Yesu hakupoteza muda alilitoa pepo
 
Kuwa umeokoka peke yake haitoshi, Yesu aliwapa siri katika mstari wa 21, kuomba peke yake haitoshi, bali ni kuomba na kufunga, ili hili litokee mpaka uombe na kufunga, unapo omba na kufunga unapata Nguvu za Mungu zaidi. Kama huna Nguvu za Mungu utakemea pepo nalo pepo litakuangalia tu, kwahiyo ili kupata nguvu za Mungu ni lazima uombe na kufunga. Kwahiyo wakati wote ni lazima uwe na ratiba ya kufunga na kuomba.

 Kuna watu wanakuja kanisani wanapenda kuimba tu lakini hawajaokoka, sasa ni lazima waokoke na wawe na tabia ya kusoma Neno la Mungu na kuomba ili wapate Nguvu za Mungu. Yesu alisema tutaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya yale aliyofanya, lakini hatutaweza kufanya hivyo kama hatuna Nguvu za Mungu ndani mwetu. 

Kwenye kanisa sasa kuna magonjwa na magonjwa hayo hayawezi kutoka mpaka watu waamue kufunga na kuomba. Na ukiona umekemea pepo na likagoma kutoka ,shida sio Yesu bali ni wewe ambaye huna Nguvu za Yesu ndani mwako.  

Unapookoka unatangaza vita na shetani, sasa usipoomba na kufunga shetani atakutesa. Unakuta mtu aliyeokoka ana shida kuliko yule asiye okoka. Mkemee shetani, usikate tamaa funga na kuomba, Yesu alisema hii isingewezekana mpaka kwa kuomba na kufunga, sio kuomba au kufunga bali ni kuomba NA kufunga.

 Kuna watu mnapigwa na shetani na kupata shida nyingi ni kwasababu mmetangaza vita na shetani wakati unapo okoka lakini huombi wala hufungi ndomana unapata shida. LAZIMA UWE NA MAISHA YA KUFUNGA NA KUOMBA, ISIPITE WIKI NZIMA BILA HATA KUFUNGA SIKU MOJA.No comments:

Post a Comment