''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, November 10, 2013

MATUKIO YA LEO

 UJUMBE: SIMAMA IMARA KATIKA MAISHA YAKO YA UKRISTO
MHUBIRI: Mch. Mhini
MAANDIKO: 1Wakorintho 10:12

Kama unazani uko imara simama imara. Neno la Mungu linakuonya kuwa usimame imara, sasa hivi kuna technelogia iliyoendelea sana sasa tuwe makini na haya maendeleo yasije yakatuharibu, tusimame imara. Dunia ipo kwajili ya kukunyonya, kuwa makini kuwa imara muache Roho Mtakatifu akufunulie, kama huna Roho Mtakatifu maisha yako yatakuwa hatarini sana. Tafuta sana kuwa na Roho Mtakatifu muda wote.

Kwanini tusimame imara?

 Dunia tuliopo imechafuka, Yesu alitumia maandiko kumshinda shetani Je wewe kwa mahali ulipo unamshinda shetani kwa kutumia nini?? 

Kwenye hii dunia ili kumshinda shetani inabidi usome Neno la Mungu kwa bidii na kuomba kwa bidii, hebu kuwa makini muda wote, kuwa mtu wa maombi na kusoma neno hapo ndio utaweza kumshinda shetani. shetani ni mjanja sana sasa kama hauombi au husomi Neno la Mungu shetani atakudanganya. Na wakati unapoweka upenyo shetani unajiingiza kwanini?? Ni kwasababu uko busy hauna muda wa kusoma Neno la Mungu wala kuomba. 

Warumi 1:17 " Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani."
Kama hakuna imani hakuna haki, na hakuna imani hakuna haki, kwahiyo uaminifu ni muhimu sana, na hauwezi simama imara kwasaabu wewe sio mwaminifu, unachukulia mambo kirahisi rahisi tu, umeokoka muda mrefu lakini inashangaza muda wote huo haubadiliki, haujali muda wote huo upo upo tu,

Ushindi haupatikani kwa nguvu zetu wenyewe bali kwa Yesu kristo, huu wokovu tuliona ni zawadi kutoka kwa Yesu kwahiyo kama tunataka ushindi lazima tuwe na Yeye

 Usiruhusu dhambi kutawala maisha yako, ndio labda haunywi pombe lakini kwa namna flani unafanya dhambi na labda kuna mambo flani unafanya kwa siri sana lakini unatenda dhambi, sasa Yesu anakuangalia sana kwa umakini. Unaweza ukawa unafanya dhambi kwa siri sana bila mtu mwingine au mchungaji wako kukuona lakini kumbuka huwezi kujificha Yesu asikuone, kwahiyo acha kufanya dhambi na badala yake simama imara. 

Unawezaje kushinda dhambi ni kwa maombi na kuwa mnyenyekevu machoni pa Mungu, ishi maisha matakatifu mbele za Mungu usifanye kitu kwasababu mchungaji atakuona bali ishi maisha matakatifu kwasababu ya Mungu. 

Uwe katika nafasi ya kumkemea shetani na kumfukuza katika maisha yako, lakini ili uweze kumkemea shetani kuwa imara na mtakatifu bila hivyo ukimkemea hata ondoka. Ufunuo 3:15-17, Hali ya kanisa la laudekia ilikuwa ya kutisha na hali hiyo ni kama ya kanisa la leo, kanisa la leo limekuwa vuguvugu, ni afadhali uwe moto au baridi lakini ukiwa vuguvugu ipo siku Bwana atakutapika, na ukiwa vuguvugu unakuwa kizuiizi katika maombi. Umekuwa mtu wa kusema sema ovyo, 

Leo unaonywa usisengenye, mpende jirani yako na simama imara, usitende dhambi, kila kinachokuzunguka kimtukuze Mungu kwasababu ya wewe, jirani zako wajifunze utakatifu kutoka kwako. 

NI ONYO USITENDE DHAMBI, IPO SIKU KILA KITU KITAWEKWA WAZI NA KUTAKUWA HAKUNA NAMNA NYINGINE YA KUTUBU,  TUBU SASA NA UFANYE MABADILIKO. SASA FIKIRIA KATIKA UFAHAMU WAKO, NI MATENDO GANI HAYAMPENDEZI MUNGU NA UNAYAFANYA HAYO KWA SIRI KUBWA NA ROHO MTAKATIFU ANAKWAMBIA YAACHE?, JE UNAONGEA VIPI NA JIRANI ZAKO? JE UNAONGEA NAO VIZURI? SAMEHE, 

Je kiko chochote amabcho hakimpendezi Bwana? Basi tubu sasa
------------------------------------------------------------------------------------------------------------

No comments:

Post a Comment