''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, November 3, 2013

KUEPUKA ROHO YA KUJIHURUMIA



 MHUBIRI: MCH. PETER MITIMINGI
MAANDIKO: 1Wafalme 17:1-16

        1Wafalme 17:1-16
1 Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu. 2 Neno la Bwana likamjia, kusema, 3 Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani. 4 Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. 5 Basi akaenda akafanya kama alivyosema Bwana; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani. 6 Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.

7 Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi. 8 Neno la Bwana likamjia, kusema,9 Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe. 10 Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa. 11 Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. 12 Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.

13 Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.14 Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi. 15 Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi. 16 Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya.

MAMBO 5 TUNAYOJIFUNZA KUTOKA KWA MAMA MJANE

1.   Mungu anamtuma Eliya kwenda kulishwa na mtu asiye na chakula.
a.   Tulimtarajia Mungu kwenda kumtuma Eliya kwa moja ya matajiri wakubwa wa Sarepta wenye hazina kubwa ya Chakula.

b.   Mungu huwatumia watu wa kawaida sana katika kutenda mambo makubwa ili aweze kujitwalia utukufu.
Mfano:
Wanafunzi wa Yesu wengi wao hawakuwa na kisomo.

c.    Mungu anaweza kukutumia wewe hata kama unajiona huna viwango vinavyotamkwa au kutajwa katika hadhi ya kibinadamu.

2.   Mungu hutazama Utayari na Utii wako kwanza kabla ya kuachilia mafuriko ya Baraka zake kwako.
a.   Eliya alitumwa na Mungu aje kula chakula kwa mjane, kwanini alianza kwa kuomba maji badala ya kueleza kile Mungu alicho mtuma?

1Wafalme 17:9
9 Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe.

1Wafalme 17:10
10… akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.

b.   Iliokuwa ni kipindi cha ukame. Maji ilikuwa ni bidhaa adimu sana ambayo isingepaswa kutolewa hovyo hovyo.

c.    Mama mjane alikuwa tayari kuyatoa hayo maji kidogo adimu kwajili ya mtumishi wa Bwana.

3.   Mungu anataka tumshirikishe tulivyonavyo hata kama ni vidogo kiasi gani hivyo hivyo.

Mungu hataki vingi usivyonavyo, bali anataka vijache ulivyonavyo.

1Wafalme 17:11-12
11 Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. 12 Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.

4.   Kujihurumia ni kizibo cha kuzuia Baraka za Mungu zisikufikie katika maisha yako.
a.   Mama mjane alikuwa na haki kabisa ya kujitetea kwamba mimi ni mjane na nina mtoto ndio tungekula kwanza kabla yako. Lakini aliondoa roho ya kujihurumia na kuamua kumtii Mungu kwanza.

b.   Hata kama unashida na mahitaji mengi kiasi gani, hakikisha unamtanguliza Mungu kwanza kabla ya kutangulisha mahitaji yako.

Mathayo 6:33
33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

5.   Tunapofanya kama Mungu anavyoagiza, tunafungua bomba la Baraka za Mungu katika maisha yetu kwa muda mrefu.

1Wafalme 17:15 - 16
15 Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi. 16 Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya.

a.   Pipa la Unga linawakilisha mahitaji yetu ya mwili
·        Hatutapungukiwa chakula
·        Hatutapungukiwa Mavazi
·        Hatutapungukiwa Malazi
·        Hatutapungukiwa Afya
·        Hatutapungukiwa Elimu
·        Hatutapungukiwa Mahitaji mbali mbali tuliyonayo

b.   Chupa ya mafuta inawakilisha Kibari kutoka kwa Mungu.
·        Maisha yetu ya kiroho yatabarikiwa
·        Mafuta ni kupata kibali na neema kwa Mungu na wanadamu
·        Mafuta ni upako wa kumenda Mungu na kumtumikia vema.


No comments:

Post a Comment