UJUMBE: MPANGO WA MUNGU KWAKO NI WA KIBINAFSI
MAANDIKO: Kutoka 3:1-22
MHUBIRI: Mch. Kiongozi Meshark Mhini
Mungu ni wa binafsi, anashughulika na wewe kama wewe, anashughulika na wewe kama mtu binafsi, ndomana ile siku ulivyompokea Bwana Yesu na kuokoka wewe binafsi ulikiri.
Sasa kuna utaratibu maalumu kabisa wa Ki-Mungu kwa ajili yako, na hiyo inamaanisha kuwa Mungu ana mpango kamili na wewe binafsi. Mungu ni wa kibinafsi sana, tunapokuwa kwenye ibada kila mtu anapokea Neno la Mungu kwa aina yake na kila mtu ana mtazamo wake na huwa ni tofauti na mwingine. Mungu anashuhulika na mtu binafsi binafsi, kadhalika Mungu ni yule yule lakini sisi hatulingani, mahitaji yetu yanatofautiana, na wewe kama mtu binafsi ni wa kipekee sana.
Kutoka 3:1-22, Tumesoma mlango wote ili kujua kwanini Mungu aliwahurumia wana wa Israel, Mungu alikuwa na mpango kamili wa kuwaokoa wana wa Israel. Yawezekana unapita katika hali nguvu mno lakini tambua Mungu ana mpango na wewe na leo ndio siku ya kufunguliwa kwako amini tu. Pia kutokana na maneno ya mlango huu, tunajifunza mambo saba (7) ya muhimu:
1. Mungu ni Mtakatifu
2. Mungu ameona mateso ya watu wake
3. Mungu alidhamiria/kuzingatia kuwaokoka watu wake
4. Mungu alichukua jukumu la kuwa pamoja na Musa
5. Mahali pa kuabuduia, lazima ujue sehemu ya kuabudia wewe mwenyewe
6. Mungu alijitambulisha Yeye ni Niko
7. Mkono wake wenye Nguvu ulikuwa na musa
Hembu jiulize, Je unatambua mpango wa Mungu kwako?, je unafahamu nafasi yako ya kumtumikia Mungu?, Mungu ametupatia karama nyingi Je unajua Mungu amekupa karama gani?. MUNGU NA AKUFUNULIE KWANINI MUNGU AMEKUUMBA KATIKA HII DUNIA na NINI ANATAKA KUFANYA.
Anafahamu kesho yako, ni wewe uwe karibu na Yeye, ukiwa mbali naye Mungu hatakufunulia siri, lazima uwe karibu naye. Musa alikaribia kile kijiti kilichokuwa kinawaka moto. Ndugu chukua hatua piga hatua zaidi na zaidi ya kuwa karibu na Mungu na ndipo utakapoisikia sauti Yake. Kila mtu ametengwa kwa kazi maalumu, Mungu amekutenga wewe kwa kazi maalumu kabisa kuwa karibu naye ili ujue ni nini anataka ufanye. Mungu anafanya kazi na wewe yohana 6:14 Mungu yuko pamoja na wewe, Mungu anaweza kukuita wewe katika huduma lakini hawezi kukuacha hivyo hivyo atakupa mahitaji yako, Mungu ana huruma sana na anakupenda sana.
MUNGU YUKO UPANDE WAKO NA MPANGO WAKE UKO KIBINAFSI KAMA WEWE UNAVYOHITAJI, MUNGU HATAKUACHA UKOSE CHAKULA, MUNGU ANA MPANGO KWA AJILI YAKO, NA MUNGU ANA HURUMA SANA, WEWE NI MTUMISHI WA MUNGU JE UNATAMBUA NI UTUMISHI GANI MUNGU AMEKUITIA? NI MUDA WA KUMKARIBIA MUNGU ILI UFAHAMU NI WAPI UNAPOTAKIWA KUMTUMIKIA.
No comments:
Post a Comment