MHUBIRI: MR. OKECH
SOMO: Kutoka 4:2, Kutoka
14:13
Je, ukiwa na maono ya
mwaka huu ni nini hasa ungependa kutekeleza?, Leo chukua muda andika kwenye daftari mambo yote unayotaka kutimiza katika mwaka huu
na uandike gharama zake.
MALENGO KATIKA ELIMU
Ili maono yako
yatimie unahitaji elimu kwahiyo ni vema uweke malengo utakavyojielimisha wewe,
watoto wako, ndugu zako. Elimu ni kitu
cha lazima, haijalishi ni elimu gani, kune elimu ya kuipatia shuleni lakini pia
kuna ile ya kujifunza kutoka kwa watu.
MALENGO KATIKA
BIASHARA NA KAZI
Uzembe na Uvivu ni adui mkubwa sana wa maendeleo. Mambo
ya uzembe na uvivu yasitajwe tena kwenye maisha yako, na kuna watu hawana cheti
chochote na hawana kazi lakini usijikie kwamba Mungu amekusahau Mungu anajua
hilo, ni jukumu lako wewe kuweka mambo yako sawa. Musa aliulizwa na Mungu una nini mkononi na
akatumia fimbo hiyo hiyo kuokoka wana wa Israel.
Pia kwa wafanyakazi
ni muhimu sana kufungua biashara yako ya binafsi LAKINI chagua biashara ambayo
haitakuwa na muingiliano kwenye kazi zako ili kuepusha majaribu, biashara yako
isipunguze ufanyaji kazi wako kazini. Ukiamua
kufanya biashara kuwa nayo “serious”.
Kila mtu amepewa karama na huduma yake, Mungu amekupa kitu
cha kufanya, Amua kitu ulichopewa kufanya kwa bidii, hata kama una kazi yaaani
upo kazini, usisubiri mpaka jumapil fanya kazi ya Mungu muda wowote unaoupata.
Pia katika familia ni muhimu sana wana ndoa kuamabiana
malengo yao,. MTAZAMO WAKO KATIKA MAISHA HAYA YANAWEZA KUFANYA UFIKE AU USIFIKE
KATIKA MAONO YAKO, inategemea unaona maisha
yako yapoje, unapotazama maisha yako, kile Mungu alichokupa katika maisha yako,
ukijiona kama panzi mbele ya majitu utabaki kuwa panzi hivyo hivyo lakini ukiwa
na mtazamo wa joshua na kalebu wa kuwaona majitu si kitu utashinda, haijalishi
upo katika hali gani au una masiha gani lakini inategemea wewe unajiona kama
nani, kama mwanafunzi ukijiona wewe ni mtu wa kufeli utaendelea kufeli lakini
ukijiona ni mtu wa kufaulu utafaulu tu.
Mr. Okech akiwa anahubiri |
Mr. Okech akiwa anahubiri |
Watu wakiombewa Mungu awafanikishe kutimiza maono yao |
Familia ya Zayumba ikimshukuru Mungu kwa kuwaponya na ajali ya moto |
No comments:
Post a Comment