''Badilisha Maisha yako kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wa Maisha Yako.''

Sunday, January 12, 2014

UJUMBE: SISI NI BARUA YA YESU KRISTO KWA ULIMWENGU WOTE
MHUBIRI: Mr. Mwalongo
MAANDIKO: 2 Wakorintho 3:3
 
 Sisi ni barua sio kwa familia tu au kwa wafanyakazi wenzetu tu bali ni kwa ulimwengu wote.  Tunaweza kujifunza kwa Paulo baada ya kumpokea Yesu alipeleka injili katika miji mbali mbali. Elewa kwamba ulimwengu wote unasoma ile barua ya Kristo, sasa kwanini mnafanya tofauti? mpaka imefikia mahali ulimwengu unakusoma wanakuta mambo ya kristo na mambo yasiyo ya Kristo ndani yako wewe uliyeokoka, sasa kwanini hauwi mtakatifu?

 Wewe ni barua ya Kristo uliyoandikwa kwa Roho Mtakatifu, Paulo anawaomya wakoritho ninyi ni barua ya kristo lakini kwanini unaenenda tofauti, mwanzo ulikuwa unasomeka vizuri lakini sasa umebadilika, ulimwengu unapowaangalia unasomeka vibaya, Roho Mtakatifu yuko wapi?, paulo alikuwa analia kwanini wakoritho hawasomeki.  Kuwa barua ya kristo ni zaidi ya kuwa mtu wa kawaida, Rohi Mtakatifu sasa anakuangalia wewe na mimi kwamba Je wewe bado ni barua ya Kristo?

 Roho Mtakatifu hana furaha na wewe amehuzunishwa na wewe, hausomeki kila kitu ni dhambi umetenda dhambi. Una mambo machahe ya Yesu na Una mambo mengi ya shetani, uzinzi biblia imesema uzinzi usitajwe kwenu lakini sasa hivi unatajwa kwenu. Watu hawatoi fungu la kumi.  Barua ya Kristo haiwezi kuwa na wizi na kama ina wizi hiyo. Barua haisomeki tena, ukiangalia siku hizi watu wanasema vibaya kuhusu watu waliookoka.

NDUGU ZANGU UJUMBE HUU NI KUHUSU TOBA NA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, KATIKA MWAKA ULE WA 2013 DHAMBI NYINGI ZIMETENDEKA LAKINI MWAKA HUU 2014 KUWA MTAKATIFU, ujumbe huu unakuja kwako leo Roho Mtakatifu ana uchungu mwingi sana na shetani yuko pale na yeye ndio mshitaki wetu na unapoomba shetani anamwambia Mungu huyu mtu anayeomba usimjibu huko dunia kwasababu hasomeki tena ni kweli anaenda kanisani lakini sio mtakatifu tena. Tumeaanza mwaka mpya sasa lazima tuanze ukurasa mpya, mwaka huu 2014 lazima tuanza upya ni lazima usomeke kama husomeki ni bora uondoke, ni lazima barua zote zisomeke haziwezi kuchanagnyika na ambazo hazosomeki



No comments:

Post a Comment