YATUPASA
KUWA NA UKIRI WA WAZI MBELE YA MATAIFA
Kwa kuwa wokovu wa Yesu Kristo ni njia kuu ya
kuingia katika Ufalme wa mbinguni, kwa kila anayeliamini Jina la Yesu, habari
zake zitanenwa kwa mataifa yote kwa ujasiri wote. Kwa kuwa anayekusudia kunena
habari za Yesu, anao ushuhuda juu ya Yesu Kristo; huwa ni shahidi ambaye
anasimamia kweli yote. Mtume Paulo alikuwa na ujasiri wote wa kumkiri Yesu
mbele za mfalme Agripa.
Maelezo ya msingi ya
Paulo mbele za mfalme Agripa ni ushuhuda wa kuitwa kwake na Yesu Kristo, kwa
jinsi ambayo alitokewa adhuhuri ile akiwa anatekeleza agizo la Wakuu wa
makuhani kwenda Dameski kuwapeleka na kuwatesa watakatifu walioliamini jina la
Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. (Mdo 26:
1-32). Naye mfalme Agripa alikuwa tayari kusikiliza ushuhuda wa Paulo.
Paulo akasema “Kwa hiyo Ee mfalme Agripa sikuyaasi
yale maono ya mbinguni, bali kwanza niliwahubiri wale wa Dameski na Yerusalemu
na katika nchi yote ya Uyahudi na watu wa Mataifa kwamba watubu na kumwelekea
Mungu wa kuyatenda matendo yanayopatana na kutubu kwao”. (Mdo 26: 12-20).
Vitisho vya mfalme
Agripa kwamba usomi wake umempa wazimu wa kumgeuza akili. (Mdo 26: 24). Jibu la Paulo ni la ujasiri kwamba “Sina wazimu Ee Festo mtukufu
bali nanena maneno ya kweli na ya akili kamili”
(Mdo 26: 25). Agripa kwa hoja yenye nguvu ya
Paulo anakwepa ukweli huo ambao ungemgeuza kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi
wake. Kuchomwa moyo kwa mfalme Agripa kulimpa ukweli kwamba Wokovu u-katika
Yesu Kristo pekee. Agripa hakuona kosa kwa Paulo, ambalo lingempasa apelekwe
mbele kwa Kaisari.
Tunajifunza kwamba
vitisho vya mtawala wa ulimwengu ambaye ndiye shetani havitakoma. Imewapasa
waamini kumtangaza Yesu Kristo kwa ujasiri wote katika mapito mbalimbali
magumu. Paulo aliingia Rumi na kuhubiri huko.
Ingewezekana kabisa
kwa Paulo kukubali desturi za Kiyahudi, kwani alikuwa ni Farisayo. Lakini
alisimamia kweli ya Yesu Kristo aliyemwokoa, na kumwagiza kuwaendea mataifa.
Paulo alikaa kufungoni miaka miwili – aliutumia muda huo kuandika vitabu – Waefeso,
Wafilipi, Wakolosai, na Filemoni mnamo 63 BK. Baadaye aliachiliwa huru. Na
baadaye aliandika ITimotheo, na Tito, na kifungo cha pili aliandika 2Timotheo.
Aliuwawa 67 BK.
No comments:
Post a Comment