UJUMBE: UTII
Mhubiri: Mary Emili
Maandiko: Waefeso
6:1-9, Wakolosai 3:18-22
Unapotii unapata baraka
nyingi kutoka kwa Mungu. Kuna aina nyingi za kutii, 1.kuwatii wazazi, 2.kuwatii
mabwana zetu.
Unapotii wazazi unapata
miaka mingi ya kukaa au kuishii hapa
duniani. Unaweza kujiuliza kwanini kuwatii wazazi? kwasababu ni amri kutoka kwa Mungu yenye
ahadi kumbukumbu 6:24
Pia kwasababu ukiwatii
Mungu ameahidi kutubariki kumbariki mtu anayetii wazazi wake kumb 5:16,
unapotii wazazi unapata baraka kutoka kwa Mungu, hasara ya kuacha kuwatii
wazazi ni kunapelekea kuvunja amri nyingine kama mzazi akisema usiibe usipotii
utaenda kuiba na utakuwa umevunja amri ya kutokuiba. Pia utapata miaka michache
yenye hasara,
2. Kuwatii mabwana
zetu, kama wewe ni mfanyakazi unatakiwa uwatii mabosi wako yawezekana wanakwaza
sana lakini unatakiwa uwatii hata kama wananyanyasa, unatakiwa ujitaidi kuwatii
si kwa jinsi ya mwili au hofu bali kwa kumtii
Kristo. Lakini pia mabwana wawape watumwa wao haki yao sio kwaajili yetu ni kwa
ajili ya utukufu wa Bwana Yesu, wape
wafanya kazi wako haki zao mkijua kuwa na ninyi mna Bwana wenu mbinguni,
wakolosai 4:1. Kama umemuajili mtu hata dada wa nyumbani usiwanyanyase, na hata
kama umeajili wafanya kazi ofisini wape posho zao kwa muda unaotakiwa
Jinsi utii unavyoweza
kuleta mafanikio
Ukitii Neno la Mungu utapata mafanikio, Mungu anaweza kutumia
watumishi wake kukuletea ujumbe, ukitii utapata faida lakini usipo tii utapata
hasara kubwa sana, kwa mfano Mfalme Sauli aliambiwa akaangamize waamaleki wote
na kila kitu chao, yeye akafanya kama alivyoona yeye na hakuwaangamiza wote
akamuacha mfalme wa amaleki Bwana akamuondolea Ufalme kwa kosa hilo tu. Kosa
lake lilikuwa kufanya alivyoona yeye, Je wewe huwa unatii? Au unafanya kama
unavyoona wewe?
Miss Mary Emili |
No comments:
Post a Comment