''People are being transformed into Jesus Christ through faith and the word of God''

Sunday, June 8, 2014

SIKU YA PENTEKOSTE!!

Ujumbe: Roho Mtakatifu Ni Dira Ya Maisha Ya Mwamini
Mhubiri: Mchungaji Kiongozi Mhini
Maandiko: Yohana 14:16-31,

Yesu alituachia msaidizi amabye ni Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu atakaye kaa ndani yako milele na milele, amekuja ili akae ndani yako milele. Roho Mtakatifu alikuja kwa ajili yako. Wanafunzi hawakuelewa kuhusu Roho Mtakatifu mpaka ilipofika ile siku ya pentekoste. Roho Mtakatifu ndie Roho wa kweli, na huyo roho wa kweli hukaa ndani yako. 

Petro alipojazwa akaenda kuhubiri na watu elfu tatu wakaokoka, Matendo 2:14-17, Yoeli 2:28. Siku ile ya Pentekoste mataifa walishangaa wakajua wanafunzi wa Yesu wamelewa lakini Petro akawaambia hawajalewa bali wamejazwa na Roho Mtakatifu, leo ni siku ya pentekoste duniani kote. Roho Mtakatifu hachagui kabila, ukoo, rangi, nchi, Yeye anamshukia mtu yeyote aliye kuwa na utayari. 

Roho mtakatifu ni nafsi iliyokamili yenye uungu ndani mwake, Roho Mtakatifu ana fikiri,ana hisi ukitaka kufanya kinyume na Mungu anakwambia, pia ana utashi ana uwezo wa kupenda, kuleta furaha, Roho Mtakatifu hazuiliki ukimuhitaji popote ulipo ukimuhitaji anakuja, wala hana mipaka ukimzuia ni wewe ndio umemzuia 2Petro 2:4, Yeye anatakasa nafsi shetani akitaka kuleta uongo anakwambia usidanganye, anakuelekeza anakwambia usifanye hivi. 

Nguvu ya Roho Mtakatifu itaendelea kufanya kazi mpaka Bwana Yesu atakaporudi. 1wakoritho 6:19, Roho Mtakatifu huwaonya, huongoza, huelekeza mema, ni msaada katika kumwabudu Mungu, ni mwombezi, anafundisha, anaongoza, yeye anakuwezesha na anakupa mzigo wa kazi ya Mungu, matokeo yake ni nguvu ya kushuhudia Neno la Mungu, Yohana 1:32-33, kusudi la Mungu ni kila aliyeokolewa apate Nguvu ya Roho Mtakatifu ili akamtangaze Yesu, akatangaze injili, pia Roho Mtakatifu ndie anayegawa kazi, nguvu yake si ya kukaa tu bali ni ya kutumika, ndiye muwezeshaji, matendo 8: 14-17, Mtamani Roho Mtakatifu na ukimpata jitaidi asiondoke, lazima usome Biblia, usiwe mvivu katika kusoma maandiko, chuchumilia maombi, na usiruhusu mambo ya zamani yakujie sasa, usiruhusu dhambi iliyokutesa zamani ikurudie.
 -----------------------------------------------------------------------------------------------------------

WATU MBALIMBALI WALIOJITOKEZA KUMPOKEA ROHO MTAKATIFU 

No comments:

Post a Comment